Huenda ukapoteza ajira. Umejiaandaaje kubadilika?

Huenda ukapoteza ajira. Umejiaandaaje kubadilika?

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Habari;
Katika mambo ambayo mwanadamu yeyote haweza kupinga ni ukweli kwamba duniani inabadilika.Ni ukweli usiopingika kwamba kasi ya mabadiliko iliyopo ni muhimu sana tukajiandaa kuwa wafanyakazi tofauti sana,wajasiriamali tofauti na wafanya biashara tofauti.

Leo nataka tujadili kuhusu namna fani mbalimbali zitakavyoathiriwa na mabadiliko ya kiteknolojia.Baadhi ya fani tayari zimeshaathiriwa na kuna kazi ambazo miaka 10 iliyopita zilikuwa ni za kawaida ila kwa sasa sio za kawaida.Baadhi ya kazi hizo ni pamoja na za Upiga Chapa(Hii imebadilika kwa kiwango kikubwa),Utarishi(Mesenger) n.k.Kadiri miaka inavyoenda kazi nyingine zinaathiriwa na teknolojia kama vile kazi za ualimu,udaktari,uhasibu,uongozi,ualishaji viwandani,Siasa,n.k.

Mabadiliko ya kiteknolojia yamefanya kazi hizi ama kuwa rahisi sana kiasi kwamba kazi iliyokuwa inafanya na watu 5 sasa inafanywa na mtu mmoja au inafanywa na mashine kabisa.Ukienda katika usafiri wa Anga utaona kwamba sasa mteja anaweza kununua tiketi na kucheck in online na kufika airport na kupanda ndege bila kushughulika na mtu yeyote(Human Contact).Kwa sababu hii basi ni vyema tukajadiliana kama taifa ila tufahamu ni wapi tulipo na wapi tuendako katika misngi ya mabadiliko ya mazingira ya kazi na ajira.

Natuamani mjadal huu utachokoza mjadala mpana wa maeneo yanayohitaji maboresho ili kufanya maisha ya watu kuwa bora zaidi.

Nawatakia Mjadala mwema
 
Maisha ni maamuzi na machaguo
Ukifanya maamuzi mabaya inakula kwako
Nivyema watu kujianda vyema wakiwa kazini.
Kila siku mnaambiwa
Kijana ukipata Kazi usikimbilie kuoa kabla hujajipanga, usikimbilie starehe, usioe mwanamke asiye na Kazi au shughuli ya kumuingizia kipato.
Jifunze kuweka akiba
Wekeza kidogo kidogo
Hasahasa kwenye kilimo wekeza Ela ambayo utakuwa upo tayari kuipoteza.
 
Maisha ni maamuzi na machaguo
Ukifanya maamuzi mabaya inakula kwako
Nivyema watu kujianda vyema wakiwa kazini.
Kila siku mnaambiwa
Kijana ukipata Kazi usikimbilie kuoa kabla hujajipanga, usikimbilie starehe, usioe mwanamke asiye na Kazi au shughuli ya kumuingizia kipato.
Jifunze kuweka akiba
Wekeza kidogo kidogo
Hasahasa kwenye kilimo wekeza Ela ambayo utakuwa upo tayari kuipoteza.
Mkuu,Uliyosema yana ukweli ila pia kuna ukweli mmoja nataka nikwambie.Maisha ni machaguo na hata ukichagua hayo yote haimaanishi kwamba utakuwa kwenye right track hapana.Changamoto zitakuwepo tu.Hata hivyo lengo la mjadala wangu sio kuzungumzia machaguo tu bali ni kjadili namna mabadiliko ya teknolojia yanavyowaondoa watu kwenye ajira au kuminya fursa za ajira je tunawezaje kukabiliana na mabadiliko haya?
 
Akiba yenye mawazo mtambuka.

Nikiwa na maana ya wakati upo kazini hakikisha unakuwa na tabia ya kuweka akiba ambayo inakusaidia kufanya uwekezaji hata kama ni mdogo.

Kuna mambo mengi ya kufanya sema watu wakiwa makazini wanaridhika huku wanalalamika kuwa hawana kipato cha kutosha na wengi kusema hamna muda wa kufanya mambo mengine.

Mafanikio yanahitaji kujitoa hakuwa kitu kina kuja kwa bahati bali bahati huja baada ya kupambana.
 
Hilo suala la mabadiliko ya kiteknolojia wala risiwatishe sana wakuu coz hata hizo teknolojia znahtaj maopareta mafundi waaangaliz walinzi na kuna kazi nyingin teknolojia ya mawasiliano ilipokuwa nkazan labda watu wa posta watapoteza ajira so ajira zitapungua sana lkn wap ndo imepelekea watu mamilioni kupata ajira kuanzia wakala wa mtaani had meneja wa mtandao madereva mafundi huo n mfano aisee karibu sana teknolojia ajira ziongezeke over
 
Back
Top Bottom