Pre GE2025 Huenda vurugu na ghasia zikahamia kwa muda kwenye uchaguzi wa CHADEMA Taifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Joto la kisiasa linaloendelea kupanda kila uchwao miongoni mwa kambi hasimu za wagombea uenyekiti wa chadema taifa, huenda likaishia kuwasha moto wa ghasia na fujo kutokana na kujipiga kifua kwa kila kambi kwamba, ndiyo yenye haki na uhalali wa kushinda uchaguzi huo dhidi ya kambi nyingine.

Matokeo yoyote ya uchaguZi huu yataongeza migawanyiko, uhasama na uasi, ambao wachambuzi wengi wa masuala ya kisiasa nchini wanaeleza kwamba, chadema inakwenda kudhoofika na kua chama dhaifu sana na kilichokosa uelekeo pengine kuliko NCCR Mageuzi na CUF.

Maandalizi ya uchaguzi yenye viashiria vya vurugu, fujo na uvunjifu wa amani kutoka kwenye kambi zote mbili hasimu, vimeshuhudiwa na kuzidisha hofu ya vurugu, uharibifu na pengine maafa kwenye uchaguzi huo.

Visingizio vya udanganyifu, upendeleo, rushwa na kuzuiwa kwa baadhi ya wajumbe wa kambi hizo kuzuiwa kuingia kwenye ukumbi wa uchaguzi kwa kukosa sifa za utambuzi na uhalali wa kupiga kura, viantajwa kama ngao na sababu ya kuvuruga uchaguzi huo miongoni mwa kambi za mahasimu hao.

my friends, ladies and gentleman,
kama mdau wa siasa,
unashauri Chadema wafanye nini ili pasitokee fujo na uharibifu wakati wa uchaguzi wao kesho Jan.21.2025?

Mungu Ibariki Tanzania
 
Sema mmeandaa fujo
 
Back
Top Bottom