Bezecky
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 494
- 897
Wajumbe wengi wa Kamati Kuu ya CHADEMA wameonesha kukereka sana na baadhi ya mambo yanayoendelea kwenye Mitandao ya Kijamii hasa kwa wale Viongozi wanaojiita ni Wafuasi kindakindaki wa Mwenyekiti anayemaliza muda wake Bw. Freeman Mbowe,
Wafuasi hawa Freeman Mbowe wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kukitukana chama na kumtukana , Kumdhalilisha, kumsimanga na kumtweza kabisa utu wake Mhe Tundu Lissu ambae ni makamu wa Mwenyekiti wa CHADEMA na Mtia nia wa nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa katika Uchaguzi Mkuu wa Chama mapema mwakani.
Tayari Katibu Mkuu John Mnyika ameshatoa maelekezo yasiyo rasmi kwa Kanda ya Kichama ya CHADEMA ya Serengeti kuwa Bw. Emmanuel Ntobi achukuliwe hatua za kinidhamu haraka na chombo hicho kwani ndicho chombo chenye mamlaka ya kikatiba ya kufanya hivyo.
Na Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 makosa wanayoyafanya akina Boniface Jacob na team yake adhabu yake ni kuvuliwa uongozi au kufutwa Uanachama au vyote kwa pamoja.
Kwa upande wa Yericko Nyerere yeye mamlaka yake ya nidhamu iko chini ya Mwenyekiti wake Boniface Jacob ambae nae pia ni mtuhumiwa na Mamlaka ya nidhamu ya Jacob ni Kamati Kuu hivyo huenda kamati kuu ijayo hoja hii itaibuka na Boniface Jacob atapata anachostahili ili kuilinda CHADEMA na WanaChadema.
Uchaguzi huu huenda ukawa ndio mwanzo wa mwisho wa Chama hiki kama tu Wafuasi na Wanachama hawatakuwa na hekima na busara za kibinadamu na kiuongozi.
Soma pia Alichoandika Mnyika: Maneno ya Ntobi si msimamo wa Kamati kuu Wala CHADEMA na mamlaka ya nidhamu ya Mwenyekiti huyo yako chini ya Kanda