Hujachanjwa, hupewi huduma

Hujachanjwa, hupewi huduma

Naipendatz

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2011
Posts
5,096
Reaction score
8,234
Serikali nchini Kenya imesema kuanzia December 21, 2021 watu watalazimika kuonesha cheti kuwa wamechanjwa chanjo ya Covid 19 ili kuweza kupata huduma kwenye Ofisi za Serikali na wale ambao hawajachanjwa hawatopewa huduma.

Baadhi ya ofisi ambazo bila cheti cha chanjo Mtu hatopata huduma ni Mamlaka ya Mapato (KRA), Uhamiaji. Hospitali, Shuleni na Vyuoni, Bandarini n.k

Waziri wa Afya wa Kenya Mutahi Kagwe amesema kuelekea kuanza kwa utaratibu huo kuanzia November 26, 2021 kutakuwa na ugawaji chanjo kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi kwa siku 10 mfululizo.

"Hakuna aliyesema chanjo ni lazima lakini kama unahitaji huduma kwenye Ofisi za Serikali unapaswa kuchanja"

My take: NAISHAURI SERIKALI YA AWAMU YA 6 IWAIGE WAKENYA KATIKA HILI, ILI WATU WENGI ZAIDI WAJITOKEZE KUCHANJA
 
Taratibu maandiko ya kitabu kitakatifu yanatimia.

Tumrudie Mungu.
hakika yanatimia tukiyaona kwa macho yetu mawili..lkn bdo wapo ambao wala hawashtuki, ni muda wa kutubu dhambi zetu na kumrudis Mungu...rapture is arround the corner!!
 
Ili UFO watakaposhuka wakute mnazo signal tayari, waweze kuwatumia kama mazombi kufanya maasi kipindi cha dhiki kuu na muwe mnaonekana kwenye mitambo yao, mambo ni hadharaniiiiii....
Acha kuamini ushirikina Chief
 
Watu watalazimika kuonesha cheti kuwa wamechanjwa chanjo ya Covid 19 ili kuweza kupata huduma kwenye Ofisi za Serikali na wale ambao hawajachanjwa hawatopewa huduma.
Je wamebainisha ni huduma zipi?
Je takwimu zao inaonyesha ni asilimia ngapi ya wananchi wamepata chanjo?
 
hakika yanatimia tukiyaona kwa macho yetu mawili..lkn bdo wapo ambao wala hawashtuki, ni muda wa kutubu dhambi zetu na kumrudis Mungu...rapture is arround the corner!!
"Rapture" ilianza kusubiriwa na akina Paul 50 AD, hadi leo hii 2021 AD bado mnasubiri hiyo kitu?
 
Mbona kila kitu kipo peupe.....tatizo lenu waabudu shetani mnajiona nyinyi ndo wenye siri za mambo yote ya dunia. Kwa taarifa yako hakuna jambo litakalofanyika duniani bila Mungu kuwapa taarifa wateule wake, kaeni mkijua hilo.....
Ushirikina huo, and msimsingizie "Mungu" hata kwenye ujinga
 
Back
Top Bottom