Hujafa hujaumbika

Redey

Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
47
Reaction score
4
wanajamvi kwa mara nyingine naomba mchango wenu kimawazo. Kuanzia jtatu wiki hii nasikia maumivu makari sana upande mmoja wa shavu like shoti ya umeme au kama vile moto unaniunguza.

Nimetembelea vituo vya afya na wamenipa dawa lakini sioni nafuu. Swali langu kwenu wenyeufahamu na tatizo hili-
nini kifanyike ili kuondokana na hili tatizo, au ni wapi naweza pata uhakika wa matibabu sahii.

Natanguriza shukrani. Kweli natabika make kula hata kuongea kwangu sasa ni mateso makubwa. Weekend jema...
 
I googled it na nimekutana na majibu haya:

Source: Doctors Lounge - Neurology Answers
 
tatizo lako ni dogo njoo uombewa wengi wenye tatizo kama lako wamepona
 
tatizo lako si dogo sana kama baadhi ya wadau wanavyodhani. Kutokana na maelezo yako na taaluma yangu, tatizo lako linaitwa "trigeminal neuralgia" huwa halina maelezo ya kuridhisha kuhusu chanzo chake lakini kuna sehemu fulalni ambayo inapoguswa tatizo huanza, sehemu hii inaitwa, "TRIGGER ZONE". Matibabu yake ni kama mdau mmoja hapo juu alivyo-suggest. Tumia dawa zizazotibu mishipa ya fahamu(nerves) na zenye vitamini. (Dawa kama Neurobion forte) inaweza kusaidia, ikishindikana hapo nenda hospitali kama Muhimbili kitengo cha matibabu ya kinywa na meno, ulizia mtaalam mwenye ujuzi ufuatao(maxillofacial surgeon), au neurologist kama wazo la hapo juu. Ugua pole!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…