SoC03 Hujafa, hujaumbika

SoC03 Hujafa, hujaumbika

Stories of Change - 2023 Competition

pescop bin lucky

New Member
Joined
Jul 1, 2023
Posts
2
Reaction score
2
Tangu utotoni kumekuwa na mbinu ama michezo ambayo imetusaidia katika kutukuza kiakili hata ki fikra, uwe umekulia mjini hata kama vijijini kuna ule mchezo wa kufichama na mmoja ana tutafuta ule mchezo lengo lake ni kutukuza kiakili mtu mmoja inabidi uzisome akili za wengi ili uweze kushinda, ili kuushinda ule mchezo ilihitaji umakini na utulivu wa hali ya juu endapo utasikia mitikisiko, ama minong'ono lazima uelekee hapo maana kuna asilimia kubwa utawapata unao watafuta ili kushinda

Ajabu ni kuwa ule mchezo una fundisho kubwa kwa vijana katika utafutaji maana kijana mmoja inabidi uyajue mahitaji ya wengi unapotaka kuanzisha biashara fulani, kijana ina kubidi utege sikio na uwe mfuatiliaji wa fursa mpya zinazojitokeza ili kuweza kutengeneza njia za maendeleo

Utotoni pia tulio kulia vijijini tulikuwa tunatengeneza mitego ya kunasa ndege polini na ilikuwa inatupa furaha sana endapo ndege wakinasa, je kwanini tulikuwa tunatega mitego polini na sio barabarani? Kwasababu tulikuwa tunahitaji kunasa ndege na sio watu, vivyo basi katika utaftaji wetu sasa vijana tujitahidi kutengeneza mitego itakayo tusaidia katika maendeleo na tusitegemee sana matumizi ya nguvu kwa maana haujafa haujaumbika leo wewe dereva wa bajaji unae tegemea katika udereva wako tu kesho ukapata ajari ukakatika mguu je usipo kuwa na chanzo kingine cha kukuingizia kipato utawezaje kujitegemeza wewe na familia yako?

Kumbe sasa unaweza kuwa dereva na ukawa na mitego/miladi mingine ambayo itakusaidia wewe na familia yako sio tu kwasababu ya kuogopa matatizo hapana ni kwasababu ya kujiongezea kipato, tukifanya hivyo vijana tunaweza kujikwamua katika janga hili la ajira linalosumbua kwa sasa na hata baadae na hivo na sisi tukawa wa ajili kwa wengine. Ahsante
 
Upvote 1
Back
Top Bottom