Hujafa ujaumbika!

Hujafa ujaumbika!

X-PASTER

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
11,605
Reaction score
1,843
HUJAFA UJAUMBIKA!

attachment.php

Sofia James Mwiga

Ukimuona kwa sura, ni msichana mzuri mwenye macho ya kuvutia, lakini masikini hana raha ya maisha!

Mtoto Sofia James Mwiga (17, pichani) mkazi wa Manispaa ya Mkoa wa Tabora nchini Tanzania anaishi kwa mateso kufuatia ugonjwa wa ajabu wa kuvimba miguu hali iliyomfanya ajione mpweke machoni mwa jamii huku akishindwa kuanza shule.

Licha ya baba yake kumtafutia matibabu kwa zaidi ya miaka 10 bado hajafanikiwa kwani kila Daktari anayemfanyia uchunguzi hutoa maelezo kuwa hapa Tanzania hawezi kufanyiwa oparesheni isipo kuwa nje ya nchi ambako kuna Wataalam na vyombo vya kitabibu vya kisasa.

Kutokana na umasikini alionao baba mtu ameshindwa kumsaidia badala yake amebaki akisubiri miujiza ya mungu ishuke pengine atapata mfadhili atakaye weza kumsaidia kupata matibabu hivyo anawaomba wasamaria wema popote duniani waweze kumsaidia kuokoa maisha ya mtoto wake huyo.

Hivi sasa mtoto huyu yupo katika hospitali ya Lugalo, jijini Dar Es Salaam akisubiri atakayeweza kujitokeza na kumsadia kupata matibabu sahihi nje ya nchi, kwa mujibu wa madaktari, anahitaji operation ya kuondoa nyama hizo zilizozidi.

Mungu kama amekupa, basi kumbuka na wenye shida…!

Naamini kunamtu hapo anaweza kubadili maisha ya msichana huyu kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu!

Namba ya simu ya baba mzazi wa msichana huyu ni +255 753 916690

|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|

attachment.php

attachment.php

Attachments

  • S.J.M 01.jpg
    S.J.M 01.jpg
    15.6 KB · Views: 236
  • S.J.M 02.jpg
    S.J.M 02.jpg
    13.9 KB · Views: 244
  • S.J.M 03.jpg
    S.J.M 03.jpg
    14.7 KB · Views: 231
Mkuu Moi amejaribu Kwenda?

Wengine tuko tayari kuchangia.

Peace & Love

Respect.
 
Mkuu Moi amejaribu Kwenda?

Wengine tuko tayari kuchangia.

Peace & Love

Respect.
Mkuu mimi sina uhakika kama wamekwenda, maana hii ni email nimetumiwa na swahiba wangu.

Kuna namba ya simu hapo kaka, kama unayo nafasi basi jaribu kuwasiliana na baba mtu, labda unaweza kupata habari zaidi ya huu ugonjwa wa huyu bint.
 
Angejaribu kwenda kupiga kikombe pengine kinaweza kumsaidia. ajaribu na kwenda kwnye vyombo vy habari kuomba msaada.ni hayo 2.
 
Angejaribu kwenda kupiga kikombe pengine kinaweza kumsaidia. ajaribu na kwenda kwnye vyombo vy habari kuomba msaada.ni hayo 2.
Watu wengine hacheni kutania maisha ya watu. Huyu binti anaumwa na anaitajika kufanyiwa operation na hana pesa za kumwezesha kufanyiwa operation, wewe unamwambia aende kupiga kikombe.
 
Pole zake nyingi sana,
kweli hujafa hujaumbika bado....
 
Dah! Inatisha,
wengine labda tuchangie hela japo za matunda kwa mgonjwa maana hayo mamilioni uwezo hauruhusu.
 
Tutathibitishaje kama ni kweli? Hali hiyo inasikitisha sana hasa kama wewe mzima na unaona mwenzio anaumia. Moyo wa kutoa chochote ili kumsaidia tunao,lakini naogopa zisije ishia mikononi mwa wajanja maana watu hamuamiki c wakati wa matatizo wala wa furaha.
 
Umethibisha kuwa si kweli?
 
Jamani swala hapo ni kumchangia mtanzania mwenzetu, kijana mwenzetu. Najua wengi wetu tumechoka bt kwa kile tulichonacho tumsaidie. Tutumie hyo namba ya mzee wake! Mungu amsaidie apone!
 
Tutathibitishaje kama ni kweli? Hali hiyo inasikitisha sana hasa kama wewe mzima na unaona mwenzio anaumia. Moyo wa kutoa chochote ili kumsaidia tunao,lakini naogopa zisije ishia mikononi mwa wajanja maana watu hamuamiki c wakati wa matatizo wala wa furaha.

Watu wengine bwana! Tatizo hatujazoea technology, tulizoea kupigiwa filimbi, na la Mgambo huko tulikozaliwa, mnajikusanya na kuona vi2 live, sasa we m2 anaumwa hapo na namba kazitoa..badala upige hizo namba na kuuliza unaona kama hili tatizo limepita kwanza photoshop na kuhaririwa kwanza na wanataka utapeli.. Kam upo dar fatilia mpaka umwone sasa ndo uamini.
 
Back
Top Bottom