Songoro
JF-Expert Member
- May 27, 2009
- 4,122
- 1,021
Ndugu wana JF Utawala wa Awamu ya Nne unakaribia kufikia ukingoni na kama ilivyo kawaida ya awamu zote matukio kadhaa makubwa ya Hujuma hufanyika ili kuficha/kufunika maovu yaliyofanywa ama na watawala wenyewe kama vile Ma Rais au viongozi wengine wakuu au wasaidizi na watumishi wa kawaida wa ngazi za juu.
Kwa kuanzia mwishoni mwa Utawala wa awamu ya kwanza 1984 ilifanyika hujuma kubwa ya kuchomwa moto kwa Bank kuu ya Tanzania muda mchache baada ya Operation ya wahujumu uchumi na muda mfupi kabla ya kuhitimishwa Ngwe ndefu ya utawala wa Awamu ya Kwanza .
Hali hiyo ikarejea tena mwaka 1995 baada ya moto mkubwa uliotengenezwa kutokea kwenye Jengo la wakala wa meli (NASACO) na cha kusikitisha uliteketeza kabisa Idara ya Kodi ya wakati huo (sasa TRA) na kupoteza kumbukumbu zote muhimu kipindi ambacho taifa lilikuwa linakabiliwa na kashfa ya Msamaha mkubwa wa Kodi.
Hali hiyo haikukoma bali ilijirudia tena lakini safari hii kwenye utawala wa awamu ya Tatu moto huo iunaotokea muda mfupi kabla ya kuhitimisha ngwe ya utawala 2004 lakini huu ukateketeza Chumba muhimu cha Rais Ikulu na kila kilichokuwemo kikateketea. Pengine "kosa lakiufundi" la kutoichoma moto TRA na BOT ndio lilopelekea kulipuliwa kwa Kashfa kubwa ya EPA na msamaha wa KOdi kesi inayomkabili Basil Mramba, Daniel Yona na Grey mgonja.
Hivyo basi kwa kuwa utawala huu unaelekea UKINGONI tupendekeze njia za kufanya kuzuia HITILAFU/AJALI za namna hii ili tuwe na kumbukumbu sahihi kwa hatua muhimu siku zijazo.
Naomba kuwasilisha!!