Hujuma kwa wateja, Makampuni ya Simu yanatoa namba za simu kwa wanaotoa mikopo haramu mtandaoni

Bashir Yakub

Member
Joined
May 27, 2013
Posts
96
Reaction score
1,745
Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.

Swali la msingi ni kuwa hawa wanaokopesha wanapata wapi namba za ndugu zako, jamaa, na marafiki ambazo wanazitumia ujumbe kuwataarifu kuwa unadaiwa, umeshindwa kulipa mkopo,na maneno mengine yasiyo na staha.

Fikiria mkopeshaji ambaye si tu hajawahi hata kukuona bali hajui hata uko wapi wala unafananaje, anawezaje kupata namba ya kaka yako, dada, rafiki, mkwe, shemeji, wifi,mke, mme, mtoto wako, mfanyakazi mwenzako nk.

Na wanapata namba zile ambazo ziko active ambazo kiukweli kabisa ndio wale watu mnaowasiliana mara kwa mara.

Ni mchezo mchafu kutoka ndani ya makampuni ya simu bila shaka yoyote. Ni mchezo mchafu kwelikweli.

Ni juzi tu tumetunga Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Kanuni zake, na ni wakati huu huu haya yanatokea.

Kama wewe binafsi mkopaji hujawahi kuwapa hao wakopeshaji namba za simu za kaka yako, dada, mjonba, mke, mme, mkwe nk, na wala hawakujui ulipo tuseme hizo namba wamezipata kwa mtu anayekujua pengine, basi hakuna namna chaguo lililopo namba hizo wamezipata kwenye makampuni ya simu.

Na hata tukijifanya kuwa sio makampuni ya simu yaliyotoa hizo namba bado makampuni ya simu wana majibu ya nani katoa hizo namba kwakuwa wao ndio walezi(custodian) wa siri za simu zetu ikiwemo namba tunazowasiliana nazo za kila mmoja wetu.

Katika mazingira ambayo hata mke/ mme hajui namba unazowasiliana nazo mara kwa mara hawa wakopeshaji wanazijuaje hadi kuzitumia ujumbe wa deni na maneno ya kashfa. Ni dhahiri makampuni ya simu wana maswali ya msingi mno ya kujibu na wala tusibishane sana katika hili kutiana njaa.

Mjinga mmoja kutoka TCRA nilimueleza jambo hili akaniambia ati hao watu nao kwanini wanakopa mtandaoni bila kujiridhisha kuhusu kampuni hizo zinazokopesha.

Kwani hao TCRA hawaoni hayo matangazo ya kampuni hizo za mikopo mitandaoni. Wanachukua hatua gani kulinda watu(walaji) ili kujua wakopeshaji walio halali na wale haramu wakawafungia, na kuwakamata wahusika.

Hao watu si huweka namba zao za simu na zinapatikana muda wote. Hiyo kazi ya kuwatrack si hata wakimpa mgambo wa jiji ndani ya masaa machache anawaleta hao matapeli wote.

Yaani huyu anataka watu wajiridhishe vipi sasa.

Utaratibu wa kisheria wa kujiridhisha(Due Dilligence) kuhusu uhalali wakampuni ya mkopo ninaojua ni huu ;-

1. Mkopaji afungue online account Brela, aombe kitu kinaitwa ' COMPANY DETAILED INFORMATION" , alipie alfu 25 halafu asubiri majibu ndani ya wiki ili ndo aambiwe hii kampuni ni halali au hapana.

2. Baada ya hapo apeleke maombi rasmi BOT kujua kama hiyo kampuni ina leseni ya kukopesha.

3. Na baada ya hapo apeleke maombi manispaa husika wamwambie kama hiyo kampuni ina leseni ya kufanya biashara.

4. Na ikiwezekana apitie na TRA kupata taarifa za kikodi na returns.

Ati baada hapo ndo mtu amejiridhisha sasa, na hapo sasa ndio aombe mkopo wa alfu 30 kwenye hiyo kampuni mtandaoni . Ujinga ni mwingi sana kwa baadhi ya watendaji. Sikutegemea huyu mtu aniambie hiki kitu.

Kwani kwenye hiyo mikopo inayochukuliwa Crdb, Nmb, Nbc nk ni mteja yupi huwa anajiridhisha hata kuulizia brela kama hizo benki zimesajiliwa, au ni mkopaji yupi aliwahi kwenda BOT kujua kama zina leseni ya kukopesha.

Ninachotaka kusema ni kuwa TCRA wasijivue jukumu la kuwalinda walaji wa bidhaa zao kwa kuwaeleza mambo ya kijuha ambayo hayatekelezeki.

Hizi kampuni sijui, watu binafsi wanaokopesha mtandaoni wanadhalilisha watu wawachukulie hatua kwa kushirikiana na vyombo vya usalama. Namba zao zipo na ziko active muda wote wametega kusubiri kulipwa hela zao na hivyo kuwakamata ni rahisi.

Hawa si tu wanadhalilisha watu bali pia wanaathiri mfumo rasmi wa biashara ya mkopo kwani kampuni halali zinakosa mapato kutokana na watu hawa, lakini pia serikali inapoteza kodi.

Lakini kubwa kuliko yote TCRA iwajibishe kampuni za simu, ufanyike uchunguzi kuona nani anatoa siri za wateja kwenye haya makampuni.

Makosa ya kutoa siri za wateja yanaingia kwenye jinai. Tunataka kusikia kauli yenu haraka kuhusu Makampuni ya simu na hizi siri za wateja.

Jambo hili hatuwabembelezi ni lazima mlifanye sababu ni wajibu wenu kama Regulator. Kwani nyinyi TCRA hamkai kwenye jamii haya mambo hamyasikii ama.

Tumekaa palee tunasubiri kuona.
 
Hapa hoja ni ku deal na hayo makampuni ya mikopo yanayovujisha taarifa za mteja maana kwenye kipengele cha privacy ni kwamba kampuni haitatoa taarifa za mteja kwa third-party kwa namna yoyote lakini wanakiuka kipengele hicho.

Hapo haijalishi kampuni imesajiliwa kihalali ama kampuni kanjanja zote zinawajibika kisheria kutunza siri za mteja.
 
Serikali iiingile kati uliona wapi riba ya siku saba inafika mpaka asilimia 100 ? Humo wana weka eti na insurance pia ikifika tu siku ya tano wanaanza kudai wakati mkataba ni siku saba ! Sasa huo si ni wizi ?? sio tena mkopo.
Je hiyo insurance wanayokata ni ya nini kama wanaanza kudai siku ya tano tu ? Na je hiyo insurance wanailipa kweli ?
Hapo ndipo ninapoona logic za wakili msomi hawa jamaa wanaikosesha serikali mapato na wanaharibu biashara ya mikopo.Benki kuu mko wapi ?
 
Ile app inacopy contacts, message na calls history
Na ulikubali mwenyewe hizo permission
Ila wanadhalilisha kweli kuna bos mmoja alikopa nilikuwa pata meseji eti ameniweka mdhamini wakati sijawahi saini popote kumdhamini
 
Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.

Swali la msingi ni kuwa hawa wanaokopesha wanapata wapi namba za ndugu zako, jamaa, na marafiki ambazo wanazitumia ujumbe kuwataarifu kuwa unadaiwa, umeshindwa kulipa mkopo,na maneno mengine yasiyo na staha.

Fikiria mkopeshaji ambaye si tu hajawahi hata kukuona bali hajui hata uko wapi wala unafananaje, anawezaje kupata namba ya kaka yako, dada, rafiki, mkwe, shemeji, wifi,mke, mme, mtoto wako, mfanyakazi mwenzako nk.

Na wanapata namba zile ambazo ziko active ambazo kiukweli kabisa ndio wale watu mnaowasiliana mara kwa mara.

Ni mchezo mchafu kutoka ndani ya makampuni ya simu bila shaka yoyote. Ni mchezo mchafu kwelikweli.

Ni juzi tu tumetunga Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Kanuni zake, na ni wakati huu huu haya yanatokea.

Kama wewe binafsi mkopaji hujawahi kuwapa hao wakopeshaji namba za simu za kaka yako, dada, mjonba, mke, mme, mkwe nk, na wala hawakujui ulipo tuseme hizo namba wamezipata kwa mtu anayekujua pengine, basi hakuna namna chaguo lililopo namba hizo wamezipata kwenye makampuni ya simu.

Na hata tukijifanya kuwa sio makampuni ya simu yaliyotoa hizo namba bado makampuni ya simu wana majibu ya nani katoa hizo namba kwakuwa wao ndio walezi(custodian) wa siri za simu zetu ikiwemo namba tunazowasiliana nazo za kila mmoja wetu.

Katika mazingira ambayo hata mke/ mme hajui namba unazowasiliana nazo mara kwa mara hawa wakopeshaji wanazijuaje hadi kuzitumia ujumbe wa deni na maneno ya kashfa. Ni dhahiri makampuni ya simu wana maswali ya msingi mno ya kujibu na wala tusibishane sana katika hili kutiana njaa.

Mjinga mmoja kutoka TCRA nilimueleza jambo hili akaniambia ati hao watu nao kwanini wanakopa mtandaoni bila kujiridhisha kuhusu kampuni hizo zinazokopesha.

Kwani hao TCRA hawaoni hayo matangazo ya kampuni hizo za mikopo mitandaoni. Wanachukua hatua gani kulinda watu(walaji) ili kujua wakopeshaji walio halali na wale haramu wakawafungia, na kuwakamata wahusika.

Hao watu si huweka namba zao za simu na zinapatikana muda wote. Hiyo kazi ya kuwatrack si hata wakimpa mgambo wa jiji ndani ya masaa machache anawaleta hao matapeli wote.

Yaani huyu anataka watu wajiridhishe vipi sasa.

Utaratibu wa kisheria wa kujiridhisha(Due Dilligence) kuhusu uhalali wakampuni ya mkopo ninaojua ni huu ;-

1. Mkopaji afungue online account Brela, aombe kitu kinaitwa ' COMPANY DETAILED INFORMATION" , alipie alfu 25 halafu asubiri majibu ndani ya wiki ili ndo aambiwe hii kampuni ni halali au hapana.

2. Baada ya hapo apeleke maombi rasmi BOT kujua kama hiyo kampuni ina leseni ya kukopesha.

3. Na baada ya hapo apeleke maombi manispaa husika wamwambie kama hiyo kampuni ina leseni ya kufanya biashara.

4. Na ikiwezekana apitie na TRA kupata taarifa za kikodi na returns.

Ati baada hapo ndo mtu amejiridhisha sasa, na hapo sasa ndio aombe mkopo wa alfu 30 kwenye hiyo kampuni mtandaoni . Ujinga ni mwingi sana kwa baadhi ya watendaji. Sikutegemea huyu mtu aniambie hiki kitu.

Kwani kwenye hiyo mikopo inayochukuliwa Crdb, Nmb, Nbc nk ni mteja yupi huwa anajiridhisha hata kuulizia brela kama hizo benki zimesajiliwa, au ni mkopaji yupi aliwahi kwenda BOT kujua kama zina leseni ya kukopesha.

Ninachotaka kusema ni kuwa TCRA wasijivue jukumu la kuwalinda walaji wa bidhaa zao kwa kuwaeleza mambo ya kijuha ambayo hayatekelezeki.

Hizi kampuni sijui, watu binafsi wanaokopesha mtandaoni wanadhalilisha watu wawachukulie hatua kwa kushirikiana na vyombo vya usalama. Namba zao zipo na ziko active muda wote wametega kusubiri kulipwa hela zao na hivyo kuwakamata ni rahisi.

Hawa si tu wanadhalilisha watu bali pia wanaathiri mfumo rasmi wa biashara ya mkopo kwani kampuni halali zinakosa mapato kutokana na watu hawa, lakini pia serikali inapoteza kodi.

Lakini kubwa kuliko yote TCRA iwajibishe kampuni za simu, ufanyike uchunguzi kuona nani anatoa siri za wateja kwenye haya makampuni.

Makosa ya kutoa siri za wateja yanaingia kwenye jinai. Tunataka kusikia kauli yenu haraka kuhusu Makampuni ya simu na hizi siri za wateja.

Jambo hili hatuwabembelezi ni lazima mlifanye sababu ni wajibu wenu kama Regulator. Kwani nyinyi TCRA hamkai kwenye jamii haya mambo hamyasikii ama.

Tumekaa palee tunasubiri kuona.
Ukidownload app wanakuomba permisson ku access contacts zako na hio inakua ni lazima kisha wanapata list ya watu wote unaowasiliana nao mara nyingi
 
BORAPESA ndio wadharirishaji wakubwa,wanatuma hadi picha yako na kitambulisho chako kwa whatsap kwa watu wote uliowa-save kwenye simu yako.usijaribu.kuna jamaa anajiandaa kuwashughurikia
 
Back
Top Bottom