Huko mbinguni tutakuwa katika umri gani?

ZENITH

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
1,035
Reaction score
920
Sote waislamu na wakristu tunaamini katika maisha baada ya kifo.Pia kwa sisi wakristu tunaambiwa mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa,which means hakutakuwa na kuzaana.

Sasa najaribu kujiuliza,huko mbinguni kutakuwa na marika(umri) tofauti yaani watoto vijana na wazee,au sote tutakuwa na rika moja.

Na kama ni rika moja,je ni lipi?Utoto,Ujana au Uzee.Au ni ile age tukifa nayo ndo inagandishwa hiyo hiyo??
 
Give me your mango and i promise you will receive three more at heaven,

This is how you can convince an idiotic man who claims himself to be a great thinker,

Niongezee,
Je huko mbinguni tutaishi kama wanyama?
 
Hakuna umuhimu wa hayo yote, emu tuendelee kuishi tu
 
Hapa ndo wenye hawaamini Mungu ndo hupatia sana point kwamba Mungu ni ngonjera tu za watu[emoji3]
 
Je waliofariki wakiwa watoto au vijana mbinguni watakuwa wanakuwa(advance)? Na waliofariki wazee huko mbinguni watakuwa wazee au watakuwa vijana?
 
Mbinguni hakuna mambo mengi, hakuna hotel, ni kula mkate na divai, kuimba na kusali tu.

One more thing mbinguni ni furaha, ndo maana biblia inatueleza kuwa tusitake kujua habari za wafu, Mungu hakutaka tujue furaha iliyopo mbingu ili tuwe na hofu ya kufanya maovu tukijua mbinguni ni raha tupu.ila kiuhalisia mbinguni ni raha tupu.

Age ulokufa nayo ndo unabaki nayo ndo maana halisi ya kuzaliwa upya.

Ushawahi kujiuliza kwanini ukimuota mtu alokufa unamuota katika muonekano ule alotoka nao duniani?

Nawazaga tu siku nikifaga nikifika tu mbinguni baba yangu atakuja anikumbatie kwa furaha, shoga yangu ataniita kwa sauti my wiiiiii akifurahi kuniona, shoga yangu mery nae atanikumbati,bibi yangu yaani wote marafiki zangu watanikumbatia.baada ya hiyo furaha ya watu wangu wa karibu, ntamuona kwa mbali jpm ntaenda nimsalimie.hivyo yaan.
 
Peponi hakuna mtoto wala mzee.

Kiroho unakuwa na umri kati ya miaka 25 mpaka 35.

Hata shetani ni kijana handsome kabisa na umri wake unakadiliwa kuwa ni 30 ila tu ameamua kuwa muovu.

Satan
 
Sote waislamu na wakristu tunaamini katika maisha baada ya kifo.Pia kwa sisi wakristu tunaambiwa mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa,which means hakutakuwa na kuzaana.

Sasa najaribu kujiuliza,huko mbinguni kutakuwa na marika(umri) tofauti yaani watoto vijana na wazee,au sote tutakuwa na rika moja.

Na kama ni rika moja,je ni lipi?Utoto,Ujana au Uzee.Au ni ile age tukifa nayo ndo inagandishwa hiyo hiyo??

Usichanganye kati ya umri wa mwili na umri wa Roho, Roho haina umri na ndio maana haifi, mwili ndio wenye umri na ndio maana unakufa.

Kinachokwenda mbinguni ni Roho na ndio hiyo itahukumiwa.

Roho haina umri, Roho haikuwi, Roho haizeeki, Roho haifi.
 
Mbinguni hakuna mambo mengi, hakuna hotel, ni kula mkate na divai, kuimba na kusali tu.

One more thing mbinguni ni furaha, ndo maana biblia inatueleza kuwa tusitake kujua habari za wafu, Mungu hakutaka tujue furaha iliyopo mbingu ili tuwe na hofu ya kufanya maovu tukijua mbinguni ni raha tupu.ila kiuhalisia mbinguni ni raha tupu.

Age ulokufa nayo ndo unabaki nayo ndo maana halisi ya kuzaliwa upya.

Ushawahi kujiuliza kwanini ukimuota mtu alokufa unamuota katika muonekano ule alotoka nao duniani?

Nawazaga tu siku nikifaga nikifika tu mbinguni baba yangu atakuja anikumbatie kwa furaha, shoga yangu ataniita kwa sauti my wiiiiii akifurahi kuniona, shoga yangu mery nae atanikumbati,bibi yangu yaani wote marafiki zangu watanikumbatia.baada ya hiyo furaha ya watu wangu wa karibu, ntamuona kwa mbali jpm ntaenda nimsalimie.hivyo yaan.
Mbingu ni Human Fantasy.
 
Mkuu,Kwani wewe ni umri gani?Umri ni sehemu ya physical dimension,Ila wewe kama wewe umri wako ni mmoja tu regardless wewe ni wa miaka 90 au ni wa mwezi mmoja.Mbinguni utaingia katika hali hio hio..
 
Back
Top Bottom