Serikali ya Manispaa ya Jiji la Tokyo Nchini Japan inatarajia kuweka ratiba mpya ya kazi kwa wiki nzima kwa Wafanyakazi wa Serikali ambayo itaweka bayana kwamba siku za kazi sasa zitakuwa nne tu kwa wiki (Jumatatu, Jumanne, Jumatano na Alhamisi) huku siku za mapumziko zikiwa tatu kwa wiki (Ijumaa, Jumamosi, Jumapili).
Akizungumza katika hotuba ya sera wakati wa kikao cha kawaida cha Bunge la Metropolitan Tokyo, Gavana wa Jiji hilo, Yuriko Koike amesema sheria hiyo inatarajiwa kuanza kutekelezwa rasmi kuanzia April 2025.
Koike amesema Serikali ya Jiji hilo imepanga kufanya mageuzi hayo ili kuboresha mazingira na unyumbulifu katika maeneo ya kazi ikiwemo kuwasaidia Wanawake walio makazini kusawazisha majukumu yao ya kazi na Familia.
Tokyo imeungana na Mkoa wa Miyagi wa hukohuko Japan ambao tangu October mwaka huu ulitangaza mpango wa kupunguza wiki ya kazi kuwa siku nne tu kwa wiki kwa Wafanyakazi wote wa Mkoa ifikapo mwaka wa fedha 2026.
Sababu za Serikali nyingi za Japan kutekeleza mpango huo ni kutokana na Nchi hiyo kukabiliwa na tatizo la uzazi na kiwango cha Watoto kuzaliwa kushuka hadi rekodi ya kiwango cha Watoto 1.2 kwa kila Mwanamke.