Huku Kijiji cha Usuka, Wananchi hawaifahamu Katiba Inayopendekezwa

Huku Kijiji cha Usuka, Wananchi hawaifahamu Katiba Inayopendekezwa

mhugo hantish

Senior Member
Joined
Apr 21, 2015
Posts
137
Reaction score
36
Pamoja na kuahirisha tarehe 30.4.2015 ya kuipigia kura katiba inayopendekezwa bado vijijini kumekua na sintofahamu juu ya katiba hiyo. Nitumie fursa hii kuiomba bunge maalum la katiba kua inatakiwa zitolewe nakala za kutosha kuwafikia wananchi hasa vijijini. Baadhi hawajui kusoma hata kuandika Lakini wana mawazo ya kujenga taifa letu. Hiyo ni changamoto kwa waelimishaji.
 
Watazipata tuu kaka ucjali haya ni mambo mazuri na muhimu sana katika jamii yetu.
 
Pamoja na kuahirisha tarehe 30.4.2015 ya kuipigia kura katiba inayopendekezwa bado vijijini kumekua na sintofahamu juu ya katiba hiyo. Nitumie fursa hii kuiomba bunge maalum la katiba kua inatakiwa zitolewe nakala za kutosha kuwafikia wananchi hasa vijijini. Baadhi hawajui kusoma hata kuandika Lakini wana mawazo ya kujenga taifa letu. Hiyo ni changamoto kwa waelimishaji.

SIDANGANYIKI WANANCHI WA KIJIJI HICHO WANAISOMA NA WANAIELEWA ,Kijiji cha Usuka,kiko kata ya Usuka,Wanging'ombe,Njombe!!! Mie nimesoma post yako nikatafakri nikagundua huu ni uongo wa mchana kweupe siwezi kuuacha ukapita!kwa taarifa yako kati ya vijiji ambavyo viko active kwenye masuala ya Katiba na siasa ni kijiji hicho!

Hoja uliyoitoa ni uongo wa mchana kweupe!mtoa hoja unajaribi kupotosha umma ukifikiri utaonewa huruma au ukidhani ya kuwa kijiji hicho hakijulikani! ni moja ya vijiji ambavyo vijana wake wako makini sana katika kufuatilia masuala yanayohusu mustakabali wa taifa lao, wananchi wako very active katika shughuli za kilimo kwa kutumia zana za kisasa ikiwemo power tiller n.k. Mpaka vijana wamefikia kumiliki mashamba yao wenyewe,na kwa taarifa yako vyama vyote vikubwa vimeshafanya shughuli zao huko na ukibisha ntakupa picha na kama unavyojua katiba mpya ndo mpango mzima!!!

Wanakijiji wanajitambua na wanaendelea kuisoma katiba inayopendekezwa,acha kupotosha!!!tafuta sehemu nyingine ya kudanganya!
 
Kweli nimegundua kuna watu wanapenda kusema uongo,afadhari umemshitukia maana tulikua tumeiamini taarifa yake tukajua kweli hawajapata Katiba daaaaa ni sheeeedaah!
 
Mtu anakosa cha kuandika JF anaona bora aandike kitu cha uongo anachojiskia yeye. Kwa asilimia kubwa vijiji vyote vimeshapata Katiba zinazopendekezwa sema tu changamoto ni uchache. Lakini jamaa kaja na hoja ya kijuha hapa kuonyesha kwamba Usuka hazijapelekwa kabisa Katiba. Hata mimi napafahamu sana Usuka.
 
Wewe uko chama cha majuha,fullstop.
Mtu anakosa cha kuandika JF anaona bora aandike kitu cha uongo anachojiskia yeye. Kwa asilimia kubwa vijiji vyote vimeshapata Katiba zinazopendekezwa sema tu changamoto ni uchache. Lakini jamaa kaja na hoja ya kijuha hapa kuonyesha kwamba Usuka hazijapelekwa kabisa Katiba. Hata mimi napafahamu sana Usuka.
 
Kipengele cha 50 kwa 50 kitavunja ndoa vijijini...! Nilikuwa huko hivi karibuni....mijadala ya katiba ni mikali huko. lakini hawana wakuwafafanulia maana ya baadhi ya vifungu kwenye katiba hiyo.

Kuna sehemu, nilikuta mjadala na mada kuu ilikuwa juu 50 wanawake na 50 wanaume. Inasemekana wanawake wamejiandaa kuhakikisha mgawanyo wa kazi ndani ya nyumba unakuwa sawa. Wanasema sasa kupika, kuosha vyombo, kufua nguo lazima iwe hamsini kwa hamsini. Nilihuzunika sana...kuona washika mpini wanalazimisha kupigiwa kura katiba pendekezwa hata kabla wananchi hawajaielewa vizuri katiba pendekezwa yenyewe.
 
Umetumia lugha ya jumla bila utafiti wa kina,ati kijiji cha usuka hawajaisoma katiba pendekezwa!umejuaje hadi ukapigia mstari hivyo!ama ulitoa maswali dodoso Kwao!katiba pendekezwa inasomwa sana na inaelezewa sana walioisoma tena zaidi hata ya mijini!ile nortion ya kijijini watu hawajui mambo Futa! Sema ndiyo kwa katiba PENDEKEZWA acha kupiga ramli
 
Hahahaha tujitegemee ulihuzunika bure tu!sema umekosa muda kuwa fuatilia ukaona wanavyo ichambua katiba Pendekezwa utawakubali na wana muda mwingi tu kujadili!sasa ukiniambia ati ulihuzunishwa sikuelewi
 
Pamoja na kuahirisha tarehe 30.4.2015 ya kuipigia kura katiba inayopendekezwa bado vijijini kumekua na sintofahamu juu ya katiba hiyo. Nitumie fursa hii kuiomba bunge maalum la katiba kua inatakiwa zitolewe nakala za kutosha kuwafikia wananchi hasa vijijini. Baadhi hawajui kusoma hata kuandika Lakini wana mawazo ya kujenga taifa letu. Hiyo ni changamoto kwa waelimishaji.

Hizi ndiyo hoja za ajabu. Eti hawajiona Katiba inayopendekezwa, je iliyopo wameiona? WM
 
Hakuna sehemu nyingi tu hiyo katiba inayopendekezwa.
 
Jitokeze kujiandikisha,shiriki kupiga kura ya ndio wakati utakapofika ili tupate katba mpya.
 
Back
Top Bottom