Hukumu: Jaji asema “Wanaume ni maderava wazuri kuliko wanawake”

Ambiente Guru

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Posts
2,605
Reaction score
1,085
Jaji ametoa hukumu/ uamuzi kuwa wanaume ni madereva makini/wazuri zaidi kuliko wanawake. Hivyo, shule za udereva ni ruksa kuwalipisha wanawake ada kubwa zaidi.

Jaji Javier Albar wa Uhispania alitoa hukumu hayo baada ya kutakiwa kuamua kama kuna dhidi ya wanawake.

Wanaume hulipa Euro 665 na wanawake Euro 850.

Utafiti unaonyesha wanawake wanahitaji muda mwingi wa masomo kufaulu udereva kuliko wanaume.

Hat hivyo, Hukumu hiyo imekubwa na utata kwani taasisi za akina Mama zinajipanga kukata rufaa.


Kwetu: Traffik mmoja kule Zanzibar alionyakuwa vazi la kichwani hukwaza wanawake wakati wa kuendesha gari akatiwa matatani, sijui kama bado yupo kazini.

Emailing: Judge rules men are better drivers than women - Europe - World - The Independent
 
Nadhani shule inayohusika wali-back up madai yao kwa kuwasilisha mbele ya jaji reseach iliyofanyika na ikaonekana kwamba wanawake wanahitaji muda mrefu zaidi kuweza kujifunza kuendesha gari kuliko wanaume.
 
Mdau Macho_Mdiliko! Inawezekana, hali hii inaweza kutofautiana kutokana na tofauti za; jamii / utamaduni(mavazi, makuzi na kujiamini), mazingira ya kijiografia mfano aina ua miundombinu/ landscape na aina za chombo (malori & saloon). Pia mfumo, wakati wengine huendesha kushoto wengine huendesha kulia. Cheers!
 
Wanawake na hili nalo watasema haki sawa kwa wote, wakati hata Mungu alitufanya sisi wanaume kuwa juu ya wanawake. Mi nasema hata huko bongo walipishwe juu zaidi.
 
Halafu wanakera sana wanapokuwa barabarani, hasa akiwa mbele yako anakuwa hana maamuzi, mzito, wanayumba njia mzima, mi hunikera sana wkt ninapokuwa na haraka zangu za kuwahi miadi hasa ile inayohusiana na pesa au kukutana na kukizindua kimwana mpya!
 
Vipi kuhusu "HAWA THE BUS DRIVER" written by Richard S. Mabala?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…