Wakuu,
View attachment 473062
Nimeona kupitia Twitter ya JamiiForums wakitoa taarifa kuwa kesho ndiyo siku ya hukumu ya Kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Jamii Media dhidi ya Jeshi la Polisi na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa matumizi mabaya ya Sheria ya Makosa ya Mtandao.
Kwa maana hiyo, tarehe hii itaingia kwenye historia ambapo aidha watumiaji wa mitandao watarejeshewa uhuru wao na Mhimili wa Mahakama au ndiyo utazikwa rasmi na hatma ya watumiaji wa mitandao kubaki katika hali ya mashaka.
=======
UPDATES:
Hukumu ya Kesi ya Sheria ya Makosa ya Mtandao iliyofunguliwa na Jamii Media yashindikana kusomwa.
Sababu za msingi kushindikana kusomwa kwa hukumu hiyo hazijaelezwa.
Aidha sababu nyingine ya kushindikana kusomwa kwa Hukumu hiyo ni kutokana na mmoja wa Majaji waliokuwa wakisimamia kesi hiyo Jaji Koroso amehamishwa na kupelekwa katika Mahakama mpya ya Mafisadi.
Hukumu imepangiwa tarehe rasmi ya kusomwa kuwa MACHI 8, 2017 asubuhi saa 4.
========
HUKUMU:
Mahakama Kuu imesema Vifungu vya Sheria vilivyopingwa na Jamii Media, vipo sawa kikatiba ila imekiri sheria kutumiwa bila kanuni ni changamoto. Pamoja na kusema vifungu vipo sawa, imezitupilia mbali hoja zote za Serikali
Hoja za Upande wa Jamii Media zilikuwa ni:
1) Sheria inaendeshwa bila kanuni, hivyo inavunja haki za binadamu
2) Vifungu vya 32 na 38 vinatumika visivyo; hivyo vitangazwe kuwa kinyume cha Katiba
Mahakama Kuu yatoa mwongozo wa kesi yoyote chini ya kifungu cha 32 ya Sheria ya Mitandao, polisi lazima waende mahakamani kuomba mahakama ishurutishe mtoa huduma kutoa taarifa.
Mwanasheria Ben Ishabakaki kaeleza kuwa tafsiri ya kauli hii ya Mahakama Kuu kisheria ina maana kesi za jinai zilizofunguliwa dhidi ya [HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG] hazijafuata sheria kwa sababu polisi walitakiwa waende kwanza mahakamani badala la kukamata na kufungua mashtaka moja kwa moja.
Wamesema kifungu kipo kinachowataka Polisi kwenda mahakamani endapo watanyimwa data kabla ya hatua wanazochukua dhidi ya Jamii Media kama mtoa huduma.
Mahakama Kuu yamwonya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutohoji Mamlaka ya Mahakama katika kutafsiri sheria.
Mahakama yasisitiza kuwa sheria zilizopo zinahitaji kuzingatia maendeleo ya teknolojia na Haki ya Faragha
Mahakama imeongeza kuwa kuna umuhimu wa kuwa na Kanuni za kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Makosa ya Mitandao
"Ni muhimu kujua nani wako nyuma ya msukumo huu wa kupata data za watumiaji. Hatupambani na Dola" - Maxence Melo