Hukumu ya aliyekuwa RC Simiyu, anayetuhumiwa kulawiti kutolewa leo Novemba 29

Hukumu ya aliyekuwa RC Simiyu, anayetuhumiwa kulawiti kutolewa leo Novemba 29

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Hukumu ya kesi ya kulawiti inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (RC), Dkt. Yahya Nawanda inatarajiwa kusomwa leo Ijumaa Novemba 29, 2024, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza.

Kesi hiyo ya kulawiti namba 1883/2024, inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Erick Marley.
1732860611557.png
Mara ya mwisho kuripoti mwenendo wa kesi hiyo ilikuwa Septemba 10, 2024 baada ya kutopata ushirikiano licha ya Marley kuruhusu wajulishwe mwenendo wa kesi bila kuvunja taratibu kwa kuwa kesi hiyo ilikuwa ni ya nyuma ya kamera.

Pia, Soma: Kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Simiyu anayetuhumiwa kulawiti imeishia Wapi?

Siku hiyo shauri hilo lilitakiwa kuendelea na usikilizwaji wa ushahidi wa upande wa mshtakiwa (Dk Nawanda).

Kabla ya ushahidi wa upande wa mshtakiwa kuanza kutolewa, Julai 16, 2024 mbele ya Hakimu Marley, mashahidi wawili wa Jamhuri ambao ni mwanafunzi anayedaiwa kulawitiwa na Dk Nawanda na mama mzazi wa mwanafunzi huyo walifungua ukurasa wa kutoa ushahidi ambapo waliutoa nyuma ya kamera (faragha).
 
photo_2024-11-29_10-27-38.jpg
Hukumu ya kesi ya kulawiti inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (RC), Dkt. Yahya Nawanda inatarajiwa kusomwa leo Ijumaa Novemba 29, 2024, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza.

Kesi hiyo ya kulawiti Namba 1883/2024, inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Erick Marley.

Kabla ya ushahidi wa upande wa mshtakiwa kuanza kutolewa, Julai 16, 2024 mbele ya Hakimu Marley, mashahidi wawili wa Jamhuri ambao ni mwanafunzi anayedaiwa kulawitiwa na Dk Nawanda na mama mzazi wa mwanafunzi huyo walifungua ukurasa wa kutoa ushahidi ambapo waliutoa nyuma ya kamera (faragha).
photo_2024-11-29_10-27-39.jpg

==================
 
Hukumu ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahya Nawanda katika kesi ambayo anatuhumiwa kumlawiti Binti inatarajiwa kutolewa leo November 29,2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Ilemela chini ya Mhe Marle kuanzia saa 3 Kamili Asubuhi

Upande wa utetezi unawakilishwa na mawakili Alex mgongolwa akishirikiana na wakili Mtalemwa.

Ambapo katika hatua za ushahidi Jamhuri wao walipeleka mashahidi 11 dhidi ya Mshatakiwa (Nawanda) ambaye kwa upande wake alikuwa yeye peke yake.
Duh pole yake aya maisha bhana ..leo upo juu kesho upo shimoni.
 
Tuache kudanganyana! Kwenye hii nchi sheria zinawahusu watu wa chini tu. Na siyo wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa. Na huu ndiyo ukweli mchungu!

Hivyo huyo RC hawezi kufungwa! Na hata ikitokea bahati mbaya, bado atatoka tu baada ya muda fulani kupitia mapungufu ya kisheria yatakayo achwa kwa makusudi kwenye hukumu yake, kama ilivyotokea kwa Lengai Ole Sabaya.
 
mahakama imeshamwahia huru, hana kesi ya kujibu
 
Back
Top Bottom