sajo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,474
- 6,195
Taarifa ya Kamati ya haki, maadili na Madaraka ya bunge iliungwa mkono na Spika wa Bunge kabla ya kuanza kujadiliwa na bunge (baada tu ya Mwenyekiti wa kamati kutoa hoja). Tafsiri ni kuwa ilielekeza wabunge nini kinachotakiwa na Spika. Muelekeo ulikuwa ni kuunga mkono hoja na sio vinginevyo.
Uchaguaji wa wabunge waliochangia taarifa ya kamati.
Taarifa ya kamati ilichangiwa na takribani wabunge 10 au 11, kati yao wabunge 8 walikuwa ni wajumbe wa kamati iliyotoa hoja (iliyowasilisha taarifa). Haieleweki kama walipangwa (waliandaliwa) kuchangia, au wabunge wegine hawakuwa na maslahi (interest) kujadili taarifa au ilitokea tu coincidence kwa Mheshimiwa Spika kuchagua wabunge hao;
Je, ilikuwa sahihi kwa wabunge ambao ni wajumbe wa kamati kujadili taarifa ya kamati yao?
Ukisoma kanuni za bunge za mwaka 2020, zipo kimya, hazijaeleza kuhusu hilo kama wajumbe wa kamati wanaweza kuchangia taarifa ya kamati yao au la. Hata hivyo, mazoea (Good Practice) katika sekta tofauti (ikiwa ni pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa) ni kuwa wajumbe wa kamati husika huwa hawaruhusiwi kuijadili taarifa ya kamati yao baada ya kuwasilishwa isipokuwa wajibu wao ni kuitolea ufafanuzi pale wajumbe wasio wanakamati wanapohoji. Kilichofanyika bungeni jana ilikuwa ni kwenda kinyume na good practice kwani karibu asilimia 80 ya waliochangia taarifa walikuwa ni wajumbe wa kamati. Madhara ya wajumbe kujadili taarifa yao wenyewe ni kuwa na majibu tegemewa (expected answers), kwamba isingewezekana kwa wajumbe hao kujadili tofauti na kilichowasilishwa na wao wenyewe (hoja iliyopo mezani) maana ingekuwa ni kujikata mitama. Kwa mazingira haya ni rahisi kuhitimisha kuwa azimio la bunge la tarehe 31 Agosti 2021 lilikuwa ni la kupangwa.