Kutawadha: ima ni lazima na ima inapendekezwa:
a. Ni lazima kutawadha kwa mambo matatu
Mwenyezi Mungu U Anasema:
{Enyi Mlioamini! Mnapo simama kwa ajili ya swala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni} [5: 6]
2. Kutufu Alkaba:
Kwa kauli yake Mtume ﷺ kumwambia mwanamke aliye katika hedhi: (Usitufu mpaka utwahirike) [ Imepokewa na Bukhari.].
3. Kushika Msahafu:
Kwa neno lake Mwenyezi Mungu U:
{Hawaigusi isipokuwa wale waliotwahiriwa} [56: 79]