Hukumu ya Sabaya, Udikteta na madai ya Katiba Mpya nchini Tanzania

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
HUKUMU YA SABAYA, UDIKITETA NA MADAI YA KATIBA MPYA NCHINI TANZANIA

Huko nyuma, sisi Askofu tulionya mara nyingi kuwa nchi yetu ilikuwa imeabiri meri iliyokuwa inatupeleka katika ng'ambo ya Udikiteta na Ufashisti. Tulikemea vitendo vya watendaji kudhalilishwa hadharani katika mikutano ya hadhara na viongozi. Hoja kwamba nchi iliingia katika Udikiteta na Ufashisti katika Awamu ya Tano sio jambo linalohitaji utafiti. Hivi karibuni aliyekuwa CAG, Prof. Assad amelalamika kuwa aliondolewa katika nafasi yake kinyume cha Katiba. Kwa maneno mengine, kuna watu walivunja Katiba. Ni katika nchi za Kidikiteta tu ambako watu wanaweza kuvunja Katiba na bado wakaendelea kubakia madarakani!

Katika nchi zinazoendeshwa Kidekiteta, ni jambo la kawaida kwa Sheria, Kanuni na Katiba kutokufuatwa na badala yake vinavyofuatwa ni matamko ya kiongozi au viongozi. Katika mazingira hayo, mamlaka na cheo ndio vinakuwa Sheria. Hakuna mtu anayeweza kuhoji kama amri inafuata Sheria au inavunja Katiba katika mazingira ya namna hiyo. Kuhoji amri za Wakuu katika mazingira hayo ni kukaribisha mateso na hata kifo!

Ni watu wangapi waliwekwa kizuizini na Akaunti zao kufungwa katika kipindi kile? Ni watu wangapi ambao mali zao zilinyang'anywa kwa amri kipindi tu katika kipindi kile? Ni watu wangapi ambao walipoteza nafasi zao za kazi kwa amri tu katika kipindi kile? Ni miradi mingapi ilitekelezwa katika kipindi kile bila kupitishwa na Bunge? Ni watu wangapi waliopotea bila kujulikana walipo katika kipindi kile pasipo uchunguzi wo wote kifanyika? Ni nani zaidi ya baadhi ya wapinzani, baadhi ya wanaharakati na viongozi wa dini wachache waliojitikeza kuhoji na kuonya kipindi kile?

Sabaya ni ishara tu! Ni ishara nzuri na ushahidi kuonyesha kuwa yeye na wenzake walitumikia Serikali ya Kidikiteta iliyokuwa imevaa vazi la kidemokrasia. Alipojitetea Mahakamani kuwa alifanya matendo yake kwa kuwa alikuwa ametumwa, Mahakama isingelimsikiliza kwa kuwa Mahakama haiwezi kukubali kuwa nchi iliingia katika Udikiteta. Sabaya ni ishara tu. He is an iceberg! Endapo, ikatokea Tume Huru ya uchunguzi, wanaweza kupatikana watu wengi zaidi katika ngazi za Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa na hata Mawaziri ambao walitumia nafasi na madaraka yao pengine vibaya zaidi kumzidi hata Sabaya.

Ili haki itendeke, kuna haja ya kufanyika kwa uchunguzi wa watu wengine waliotumikia awamu ile. Jinai haifi. Kwani yule jamaa aliyevamia Clouds IFM usiku wa manane alikuwa na tofauti gani na Sabaya? Kwani ile haikuwa matumizi mabaya ya madaraka? Mbona Mamlaka ya Uteuzi iliposikia kelele za watu iliamua kumtia moyo hadharani kuwa aendelee kuchapa kazi? Yule ndugu akipelekwa Mahakamani kwa tukio lile, akijitetea kuwa alikuwa ametumwa atakuwa amekosea.

Sisi hatujadili hukumu dhidi ya Sabaya. Bali hoja yetu ni kuwa Sabaya ni ishara kuwa nchi ilikuwa inaendeshwa kwa amri zaidi kuliko Sheria, Kanuni na Katiba. Watu wenye mamlaka walikuwa hawahojiwi. Mwaka jana walitunga Sheria zilizoongeza idadi ya watu wenye kinga, yaani ambao hawaruhusiwi kushtakiwa. Katiba yetu ina udhaifu mkubwa sana. Ina mianya inayoruhusu watu kuivunja na kuinajisi. Ndio maana tunataka kuibadirisha. Sabaya ni Ishara inayotuhimiza kuandika Katiba Mpya ambayo haitaruhusu watu wachache wainajisi kujiamulia watakavyo!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

5B75A081-FE1A-469D-A8BA-C2557315B60E.jpeg
 
Nchi bado inayo yanayochukiza. Taifa linahitaji maridhiano
 
View attachment 1976640
Huyu askofu njaa ameanza Tena kuja kuharisha humu jukwaani Jana nimemsifia leo kharibu Tena njaa kitu kibaya sanaana njaa ya tumbo na akili pia
 
Angekuwa na njaa basi angeunga mkono juhudi za Chifu Hang ya ili ASHIBISHWE. Ukisikia MZALENDO ndiyo huyu sasa.

Utakuwa humjui vizuri huyo chizi walikula hela na lissu kipindi kile sasa wanahaha kuzilipa kwa wazungu mwenzie kajisalimisja kaenda kuolewa na yeye utasikia muda simrefu kaenda kuolewa huko naye aseme Hana uhakika na maisha yake tz watarudigi na mimna za wazungu
 
Huu ni UFINYU wa akili. Kajifunze kwanza kuandika.

Utakuwa humjui vizuri huyo chizi walikula hela na lissu kipindi kile sasa wanahaha kuzilipa kwa wazungu mwenzie kajisalimisja kaenda kuolewa na yeye utasikia muda simrefu kaenda kuolewa huko naye aseme Hana uhakika na maisha yake tz watarudigi na mimna za wazungu
 
Ni watu wangapi waliwekwa kizuizini na Akaunti zao kufungwa katika kipindi kile? Ni watu wangapi ambao mali zao zilinyang'anywa kwa amri kipindi tu katika kipindi kile? Ni watu wangapi ambao walipoteza nafasi zao za kazi kwa amri tu katika kipindi kile? Ni miradi mingapi ilitekelezwa katika kipindi kile bila kupitishwa na Bunge? Ni watu wangapi waliopotea bila kujulikana walipo katika kipindi kile pasipo uchunguzi wo wote kifanyika? Ni nani zaidi ya baadhi ya wapinzani, baadhi ya wanaharakati na viongozi wa dini wachache waliojitikeza kuhoji na kuonya kipindi kile?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Hakika ilisikitisha sana... Muda umeongea...
 
Back
Top Bottom