HaMachiach
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 3,417
- 6,149
Kama inavyofahamika, watajwa hapo juu walikuwa ni viongozi wa chama cha walimu Tanzania, Deus Seif akiwa katibu mkuu na Abubakari Alawi akiwa mweka hazina wa Taifa. Walishtakiwa na Jamhuri (TAKUKURU) Mei 2021 kwa kesi ya uhujumu uchumi, wizi wa fedha za walimu na matumizi mabaya ya madaraka.
Hatimaye walitiwa hatiani na Hakimu Richard Kabate na kuhukumiwa kifungo cha miezi 6 gerezani Tar 28 Juni 2022. Kwa kutumia falsafa yao ya hakuna mkate mgumu mbele ya chai walikaa gerezani Ukonga Siku 6 tu.
Si Kamishna wa Magereza wala mahakama ya Kisutu walioeleza sababu kwa nini wafungwa hawa walikaa juma moja gerezani; kisha wakaendelea kutumikia kifungo nje ya gereza na kumaliza kifungo hicho Oktoba 2022. Kilichoshangaza watu ni kwamba inakuwaje kwa makosa makubwa kama haya kutendwa na Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi eti wafungwe miezi 6 tu?
Jingine la kujiuliza, ni kwa nini Hakimu Richard Kabate kabla ya kuutafuna mfupa ambao mahakimu wenzake 3 waliushindwa na kujiuzulu kwa kesi hii hii kabla yake alithubutu kufanya hivyo?
Hukumu hii iliyosomwa tarehe 28 Juni saa 1 hadi saa 3:20 Usiku kwenye hukumu hii Hakimu Kabate aliwaonya washtakiwa wasithubutu kukata rufaa kwa kuwa hawatakutana na Kabate mwingine? Hakimu aliona nini? Na kwa nini aliwapa hukumu laini kiasi hiki?
Hukumu laini kama hii ina funzo gani kwa wizi wa mali na fedha za wafanyakazi kama walimu? Hapa inatia shaka kama mkate haukukutana na chai.
Wafungwa tajwa hapo juu, kabla ya kukata rufaa inasemekana walionana na mmoja ya wakili mashuhuri hapa nchini (jina tunalo) na akawashauri wakate rufaa kwa kesi hii na watashinda kwa kuwa kushinda kesi mahakamani hakutokani na kuifahamu tu sheria bali muhimu ni kuifahamu mahakama, sifa ambayo wakili huyo alijigamba anayo.
Jambo ambalo walilifanya na Jamhuri yenyewe haikuwa imeridhika na hukumu hivyo nayo ilikata rufaa kwa kuona kwamba hukumu waliyopewa mafisadi hawa ilikuwa ni kichekesho. Rufaa ikasikilizwa na hukumu ilikuwa itolewe tarehe 17 Februari 2023 na Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam chumba namba 4 na Jaji Ephery Kisanya.
Jaji Kisanya aliamua kuahirisha hukumu hiyo kwa sababu ambazo hakuzibainisha. Cha kuvutia ni kwamba hukumu hiyo iliyokuwa isomwe saa 4 asubuhi saa moja kabla walionekana viongozi wa dini waliokuwa wakizunguka jengo la mahakama huku wakipiga dua.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 10 Machi 2023. Umma wa walimu, wafanyakazi wa chama cha walimu, na jamii kwa ujumla wanataka kuona kwamba, au haki inatendeka au hakuna mkate mgumu mbele ya chai.
Na hii ni kwa sababu wahusika wameshikwa mkono na baadhi ya wanasiasa waandamizi na viongozi wa serikali kupeleka maombi ngazi za juu za mamlaka waonewe huruma kwa kigezo cha kwamba walipokuwa madarakani walisaidia sana kwenye ujenzi wa madarasa, ununuzi wa madawati na misaada mingine kwa umma.
Lakini ifahamike kuwa hizo fedha walizokuwa wakitumia hazikuwa zao bali zilikua fedha za walimu na hazikutumika hivyo kwa ridhaa ya walimu. Ila walizitumia kujijengea majina na kulinda nafasi zao.
Hadi leo hii, watajwa wamefanikiwa kuwaaminisha mashabiki wao wachache kwamba kwenye hukumu ya tarehe 10 Machi 2023 mafisadi hao watatoboa wakiwakumbusha wimbo wa Dar es salaam Jazz Band wa mwaka 1965 usemao “Wewe mtoto wacha kupiga mayowe, waache watu waone wenyewe”.
Wanatarajia kufutiwa hukumu ya awali wapate uhalali wa kurudi kwenye utumishi wa umma kisha kurudi Chama cha Walimu kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Jijini Tanga Machi 2023 japo tarehe bado haijabainishwa.
Kwa hivi sasa viongozi hao wanaendelea kukivuruga chama cha walimu kwa kuwatumia baadhi ya makatibu na wenyeviti wachache wa ngazi za wilaya na mikoa na baadhi ya wafanyakazi wa makao makuu kwa kutoa taarifa za uongo kwa viongozi wa serikali na mamlaka zake kuhusu chama hata kunyofoa baadhi ya vielelezo ofisini na kuviweka kwenye mitandao ya kijamii.
Usiku wa Deni haukawii kucha na jogoo awike au asiwike nilazima kutakucha, Tarehe 10 Machi 2023 sio mbali, tutajua ni nini kinaendelea.