Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
KIUMBE SICHEKE MAMBA.
Matatizo mitihani, tumekadiriwa watu,
Alo kuwa duniani, kukwepa hatathubutu,
Tumwamini Rahmani, tusikengeuke katu,
Kutu haitakiwi peponi, chuma tusafishe kutu.
Nani aweza okoka, angali ana kauli?
Kesho waweza dondoka, jifunze kwa Sauli,
Ufalme ulimtoka, sababu ya ujahili,
Alijiona amefika, kesho ika mkabili.
Jana haikuwa shida,na leo aliipiga,
Keshoye ikawa shada, loo! shada la miiba,
Akaiacha ibada, na akamuasi BABA,
Jua aso shiba bada, vigumu kushiba baga.
Sauli alosifika, kwa uchamungu wake,
Daudi aliponyeka, katika mitego yake,
Leo waweza kuwika, na kesho usiicheke,
Ya Sauli yatakufika, nguzo yako ibomoke.
Kiumbe sicheke mamba, na wala usimtusi
Tena eti wajigamba, mamba si kitu mjusi,
Ewe mwana watamba, waja bebwa kwenye tusi,
Vuka upate kutamba, kisha ulete matusi.
Njano5
0762845394