pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
Human Rights Watch, shirikika la kimataifa la kutetea haki za kibinadamu, limeiangazia Tz kuhusu ukiukwaji wa haki za kibinadamu kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba.
HRW inadai kwamba kwa muda wa miezi mitatu iliyopita wanachama wa upinzani 17 na watanzania wengine waliokashifu serikali wamekamatwa.
Huku NGO moja ya kutetea haki za kibinadamu ikipigwa marufuku na nyingine ikipokonywa leseni. Kiongozi wa waislamu Issa Ponda naye alikamatwa na kutupwa selo kwa siku tisa bila kufikishwa mahakamani, baada ya kutoa 'press confrence' akidai uchaguzi huru na wa haki.
Huku Kwanza Tv(online) ikifungwa kwasababu za kisiasa. Ila kilinichonishangaza zaidi ni kwamba wahariri wa magazeti walitishiwa na kuonywa kuhusu kuripoti habari zinazohusu kampeni za wagombea urais wa upinzani, Tundu Lissu na Bernard Membe. Majirani mnalo na inasikitisha sana kwamba mnapitia unyanyasaji wote huu na maumivu haya yote kimya kimya.
Tanzania: Freedoms Threatened Ahead of Elections