Shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch limeitolea wito serikali ya Ukraine kuanzisha uchunguzi juu ya kile kinachoweza kuwa uhalifu wa kivita, baada ya kuibuka mkanda wa vidio unaowaonyesha wanajeshi wakiwapiga risasi miguuni wafungwa wa kivita wa Urusi.
Mkanda huo ulioanza kusambaa Machi 27, unaonyesha wanaume watatu waliovalia sare, mikono yao ikiwa imefungwa mgongoni, wakitupwa chini na watu wenye silaha na kisha kuwafyatulia risasi miguuni.
Ingawa uhalisi wa mkanda huo haukuweza kuthibitishwa, uchunguzi wa shirika la habari la AFP uliliweza kuioanisha kijiografia na kijiji cha Mala Rogan, nje ya mji wa kaskazini mashariki wa Kharkiv, ambao vikosi vya Ukraine vilikuwa vimekiteka tena baada ya mashambulizi.
Mshauri wa rais wa Ukraine, Oleksiy Arestovich, amekiri kupitia chaneli yake ya Telegram kwamba udhalilishaji wa wafungwa ni uhalifu wa kivita na unapaswa kuadhibiwa. Vikosi vya Urusi pia vimetuhumiwa kwa ukiukaji tangu kuanzisha uvamizi Februari 24.
Propaganda tupu, mara oooh...wafungwa wa3 wa kirusi wametekwa na kupigwa risasi miguuni, mara oooh... video yenyewe haijathibitishwa ukweli wa chanzo chake, tuamini kipi na tuache kipi sasa [emoji848][emoji28]
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.