Humphrey PolePole anao wajibu wa kuelezea ni yapi makubwa ametekeleza kwenye nafasi ya ubalozi!

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,468
Reaction score
31,952
Kama jamii tunapaswa na tunaaswa kumuuliza kwa kina Balozi Humphrey PolePole ni mambo gani muhimu ameyatekeleza akiwa anahudumu kama balozi Malawi na ukanda wa karibiani.

Zaidi aeleze ni makubwa gani alipanga kuyatekeleza akiwa kama balozi wa maeneo tajwa na hivyo kumsaidia Mhe.Rais kwa nafasi aliyokuwa nayo.

Je kujiuzulu kwake kama ni kweli kumetokana na kukwamishwa katika vision yake ya mambo aliyotamani kuyatekekeza au ni kwa sababu ya mambo mengine?

Ni vyema na haki pia tukasikia kutoka kwake ni majukumu yapi aliyopewa wakati wa uteuzi kama balozi na kwa kiasi gani aliweza kuyaishi na kuyatekeleza majukumu aliyopangiwa .

Kwa namna yoyote ni haki yetu sisi kama wananchi ,wanazuoni na wanasiasa kuyajua kwa kina
 


Anza na mbunge wako na waziri wa sector yako
 
Mmehama kwenye hoja zake mnaanza kuhaha na vitu vingine! Jibu alichokieleza kwanza, kipo hakipo?
 
Aliwaletea mitishamba ya Cuba
 
Tulia Bwana Chawa🚮🚮🚮🚮
Ulitaka Balozi ajenge barabara au aue watu kama huyo Bibi Nyau wa kwenu??
 
Huyu tu wa ndani performance inatafutwa kwa torch vile tule wa mbali
 
Na wewe umefanya nini ili kumtetea mama yako?
 
Maccm Polepole amewajambisha mtatoa milio kutoka kwenye kila matundu ya miili yenu kudadeq.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…