Bw. Humphrey Polepole, mjumbe wa Tume ya Katiba, leo ameibua siri ya Tume kushupalia pendekezo la kuundwa kwa serikali tatu. Amesema Wazanzibar walikuja na Katiba Mpya mwaka 2010 yenye mabadiliko mengi dhidi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano yakiwemo yale yanayobainisha Zanzibar ni nchi kamili na ina Rais wake!
Mwanajopo katika kipindi cha cha Hoja cha Star TV, Bw. Joseph Leonard Mkinga akamjibu Polepole kuwa Katiba hiyo ya Zanzibar ilikuja kutokana na udhaifu wa viongozi wa Serikali ya Muungano kuwaacha viongozi wa Zanzibar kuja na Katiba hiyo yenye kuidhoofisha Katiba ya Muungano.
Mkinga pia alimhoji Polepole kuhusu idadi ya Watanzania waliopendekeza serikali tatu ambapo kwa kweli Polepole alijikanyaga tu! Suala zito kama la kupendekeza serikali tatu litatolewaje na wananchi 18,000 tu?
Hoja zote za Mkinga zina mashiko mazito na ukijumlisha na onyo la Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuhusu kuuchezea muungano--ni wazi kabisa Tume ya Katiba inataka kutuletea majanga ya 'ukabila' utakaoigawa nchi vipande na kutuletea vurugu kubwa itakayoishia sio tu kutugawa Watanzania kati ya Zanzibar na Tanganyika, lakini pia hata hao Watanganyika na Wazanzibar hawatabaki salama kama alivyoonya Mwalimu!!
Alionya kuwa dhambi ya ubaguzi itaendelea kututafuna!!! Watanzania tuwe makini, ina maana udhaifu wa viongozi wa serikali ya muungano uliosababisha viongozi wa Zanzibar kuja na katiba ya mwaka 2010 yenye kuivuruga Katiba ya Muungano iwe ndio sababu ya kuibuka na serikali tatu ambazo hatimaye muundo huo utaivunja Tanzania?
Hasira dhidi ya viongozi wa Zanzibar ndio upelekee kuivunja nchi? Ina maana tumeshindwa kabisa kuzungumza na viongozi wa Zanzibar au Wazanzibar ili kuirekebisha katiba yao ya 2010 na tukarudi kuiheshimu Katiba ya Muungano ambayo hadi sasa inaonyesha wazi Zanzibar ni sehemu ya Tanzania? Je tumeshindwa kuzungumza na sasa suluhisho ni kuibuka na serikali tatu?
Tukumbuke sababu ya lile kundi la 45 miaka ile ya 90 kuwa ilikuwa ni hasira dhidi ya viongozi wa Zanzibar kuichokonoa Katiba ya Muungano. Hoja ile iliuawa na Mwalimu kwa uwezo wake binafsi (single handedly) na nchi ikatulia! Yaani sababu sasa ya kuibuka na serikali tatu ni kukosekana kwa 'Mwalimu' wa enzi hizi?
Tujifunze kutokana na misemo ya wahenga--hasira hasara!! Samahani kwa 'mkeka' huu--nimeshindwa kabisa kuifupisha hoja hii.
Nawasilisha!!