Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Took a ride to the end of the lane………Where no one ever goes……. Ended up on a broken train with nobody I know……But the pain and the longing’s the same……. When you’re dyin’……Now I’m lost, and I’m screaming for help alone…. Relax, take it easy!
Wengine wanamfahamu kama MK14, au kitu na box! Wapo waliompa jina la Terminator au Model 101 sio Arnold Schwarzenegger hapana hapa ninayezungumzia ni The Bull Fighter! Mwamba kutoka Rwanda! Meddie Kagere! Rafiki wa nyavu na adui mkubwa magolikipa.
Kagere anachukuliwa sana kama mmoja wa hazina kubwa katika soka la Afrika Mashariki. Ustadi wake wa kipekee, mafanikio, na mchango wake katika mchezo umemfanya apate nafasi maalum katika mioyo ya mashabiki wa soka haswa Kusini mwa jangwa la Sahara. Mwamba kutoka Rwanda ana nafasi yake ya kipekee sana katika kila timu ambayo amepata kutia mguu wake.
Umaarufu wa Meddie Kagere au Terminator unaakisi ukuaji na maendeleo ya soka la Afrika katika ngazi ya kimataifa ukitazama kwa ukaribu zaidi jitihada binafsi za mchezaji husika. Ni wazi kuwa mchezo wa Soka unazidi kupata umaarufu na kutambulika barani kote, leo Yanga wakitukana na Simba basi Afrika inasimama kutazama ni nani atapasuka huko, leo Mamelodi akikutana na Kaizer Chief basi mitandaoni kutachafuka balaa. Sasa Afrika kuna wachezaji kama Kagere wanaotumia talanta zao kama mabalozi wa soka la Afrika, wakionyesha vipaji na uwezo uliopo ndani ya ukanda huu. Mafanikio ya Kagere pia yanaonesha wazi umuhimu wa uvumilivu, bidii na kujituma katika kufikia malengo katika ulimwengu wa ushindani wa soka la kulipwa.
Ni MK14 ndiye ambaye alikuwa hana masihala kabsa na lango la mpinzani, alikuwa hacheki na kima maana alikuwa hataki kuvuna mabua! Uchezaji wake ulikuwa ni mtamu sana mithili ya Kachori na bagia za mtaa wa Rufiji, magoli ya MK14 alipokuwa Simba yalikuwa yanalipa madeni yote ya mashabiki! Kile kichwa alipokipiga kwenye mechi dhidi ya Yanga kwenye msimu wa 18/19 kwa hakika alikuwa ni mkata umeme! Muondoaji wa matumaini ya wapinzani kabsa. Pasi safi kutoka kwa John Raphael Bocco ilitosha kumpa shabaha Meddie Kagere ya kuweka kichwa kikali na kuwatanguliza Simba mbele dakika ya 71.
Wachezaji wenye karma kama Meddie Kagere huwa wanakuja dunia nadra sana! Ni kila baada ya miaka 100 nipo tunaweza kumuona tena Meddie Kagere mwingine akitupatia utamu wa kuwanyanyasa wapinzani. Ni rahisi kuokota haradani kwenye mchanga wa fukwe za Ununino ila sio kumpata mchezaji sampuli ya Meddie Kagere! Terminator! Bull fighter! Model 101.
Kocha wa National Al Alhly, Pitso Mosimane aliwahi kuzungumza kwenye mahojiano kuwa kuna jitu lipo ndani ya Msimbazi linaitwa MK14 aka Terminator, na bado aliwaadabisha vyema sana kwa kuweka chuma kimoja safi. Ndanda wana historia na huyu mwamba, pasi ya Chama ilitosha kumpa nafasi MK14 kufunga bao lenye nyota tano. Bao ambalo linatibu harara, miwasho na matangotango, bao ambalo unaweza kula ugali pasipo mboga na ukashiba. Bao ambalo ukirudia kutazama usiku gizani basi hata mbu usiku huo watakupumzisha kukunyonya damu, MK14 alianza kushangilia bao lake 22 hata kabla ya kuingia wavuni (Baraka Mpenja alipata kutangaza mechi bora zaidi ya Kagere katika msimu wa 18/19).
Mtetemo wa Terminator ulikuwa ni mtetemo wa furaha na amani ya roho kama vile unakunywa mchanganyiko wa sharubati ya embe na nanasi! Umaliziaji wa MK14 ulikuwa mchungu kama vile shubiri, Meddie we Mnyarwanda wa wapi wewe!? Hakika Simba ulitupatia furaha sana Mwamba! Kumtazama MK14 akitembeza mpira ni kama kupokea hela ya uthibitisho wa pesa wakati hali ikiwa ngumu! Mtindo wake wa uchezaji ulikuwa ni kama sotojo pembeni ya Birihani huku ukitazama fiamu ya Fifty Shades of Grey, ama kutaama shughuli za Kira Noir na Evelina Darling.
Meddie Aliufanya mpira uwe mwepesi kama vile kila mtu anaweza kungia uwanjani na kufunga, aliufanya mchezo wa soka uwe mwepesi na laini sana kama vile, urojo wa Pemba. We Meddie We! Ulikuwa na mwendokasi kama kiberenge cha mwenge, na magolikipa walikuwa wamakuogopa utadhani ukoma! Ulikuwa na shabaha ya ajabu kama American Eagle! Sitosahau kile kichwa cha 5G ulichokipiga kwenye mechi ya Simba dhidi ya Namungo, zikiwa imebakia sekunde 37 tu ukatuinua wanamsimbazi kwa nguvu zote. Wanasimba tunakupenda sana Kagere! Msimbazi inakupenda sana! Huna baya na sisi! Huna deni Terminator! Goal Machine.