Hungary yailaumu Marekani kwa 'kuididimiza' Ulaya

Hungary yailaumu Marekani kwa 'kuididimiza' Ulaya

HERY HERNHO

Senior Member
Joined
Mar 4, 2022
Posts
110
Reaction score
458
Hivi sasa nchi za Ulaya zinaendelea kukabiliwa na mgogoro mkubwa wa nishati baada ya nchi za bara hilo kuiwekea vikwazo Russia kwa kisingizio cha vita vya Ukraine.

Mwaka jana, Orbán mara kadhaa amemlaumu Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky kwa kukubali kuchochewa na nchi za Magharibi na kuitumbukiza nchi yake kwenye vita angamizi na Russia.

Waziri Mkuu wa Hungary amesema wimbi la vikwazo dhidi ya Russia kama jibu kwa mgogoro wa Ukraine limeutia kwenye matatizo mengi uchumi wa nchi za Ulaya, huku Marekani ambayo ina nishati ya kutosha ya bei rahisi ikiwa mbali na changamoto hizi (zinazopitia nchi za Ulaya).
 
Attachments

  • 20230224_135517.jpg
    20230224_135517.jpg
    177.4 KB · Views: 5
Mwaka jana, Orbán mara kadhaa amemlaumu Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky kwa kukubali kuchochewa na nchi za Magharibi na kuitumbukiza nchi yake kwenye vita angamizi na Russia.
Orban ni kama Erdogan tu, sio washirika wa kuaminika....muda wowote wanakengeuka.
 
mabeberu yanararuana wao kwa wao

Putin shikilia hapohapo
Kwa sasa Putin hana madhara tena kwa ulaya!!mlisema ohoo gesi anafunga watu watakufa kwa baridi,wapi!!maisha yanaendelea tu,na nchi nyingi sasa zinaendelea kutafuta njia mbadala wa gesi ya urusi haya soko la ulaya linaenda kupotea!!Huyo hungary na uturuki kiasi fulani toka mwanzo wako upande wa putin na ndio maana ni nchi pekee ambazo zinaweka vikwazo kwa FINLAND na SWEDEN,kujiunga NATO.Putin ameshaona kuwa goma limemshinda lakini sasa atajiondoaje ni aibu!!Ndio sasa eti amemtuma CHINA,ajifanye kama mpatanishi!!NATO nao wamesema atakuwaje mpatanishi wakati tayari ana upande anaouunga mkono???
 
Watakufa na baridi hakuna gesi sasa tumegeukia matamko ya Viongozi ..Vita sio lelemama Putin alichemka sana kuanzia hiyo Vita ya kijinga..
 
Kwa sasa Putin hana madhara tena kwa ulaya!!mlisema ohoo gesi anafunga watu watakufa kwa baridi,wapi!!maisha yanaendelea tu,na nchi nyingi sasa zinaendelea kutafuta njia mbadala wa gesi ya urusi haya soko la ulaya linaenda kupotea!!Huyo hungary na uturuki kiasi fulani toka mwanzo wako upande wa putin na ndio maana ni nchi pekee ambazo zinaweka vikwazo kwa FINLAND na SWEDEN,kujiunga NATO.Putin ameshaona kuwa goma limemshinda lakini sasa atajiondoaje ni aibu!!Ndio sasa eti amemtuma CHINA,ajifanye kama mpatanishi!!NATO nao wamesema atakuwaje mpatanishi wakati tayari ana upande anaouunga mkono???
PUT IN alisema toka awali malengo ya SMO lazima yafikiwe kwanjia mbili eidha mazungumzo ama kipigo

Kwani UCHINA ndio mwanzo kuanza mazungmzo toka SVO ianze

ORBAN anajua ukweli ndio maana anausema kama ulivyo

SVO iendeleeee.....
 
Back
Top Bottom