Hunitaki sawa, lakini kwanini unitukane?

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Kuna binti mmoja hapa kijijini kwetu nilivutiwa nae, ila kukutana nae kumwomba namba ikawa ngumu sababu ya mazingira, tulikuwa tunafahamiana kwa sura.

Kwa vile ndugu yake yule binti ni rafiki yangu nikamwomba rafiki yangu namba ya yule binti, kwanza jamaa akanionya kuwa atakutukana, achana naye, mimi nikakaza fuvu nikachukua namba yake.

Picha la kutisha linaanza, najitambulisha kwa binti kupitia text, anajifanya hanifahamu, nilimwomba radhi kuchukua namba yake bila ruhusa yake, nikijaribu kumweleza mimi ni nani, alooo nilioga matusi ambayo hayaandikiki hapa na maneno ya dharau kama vile usinizoee, koma, niteme wakati sijawahi mkosea chochote, na sio kwamba namsumbua kila mara kwenye simu hiyo ndio mara ya kwanza namtext, nilishangaa sana.

Nilisubiri siku chache nikam-text tena, mwendo ni ule ule nilishangaa sana, huyo dada matusi, alimwambia nduguye, kubwa mimi balqior namsumbua, wakati akichat na mimi anajifanya hanijui.

Dada wa watu hakujua kama nilikuwa nina nia nzuri nae, nlikuwa nshaandaa bajeti ya ku-spend nae, ikiwezekana nimsajili kabisa. Kweli tangu nianze kutongoza wadada sijawahi tukanwa hivyo, kuuliza uliza kwa ndugu zake kichini chini nasikia ni mtu wa maneno/ana mdomo.

Najiuliza huyo mdada akija kuolewa, atakuja kuwa mke wa namna gani kwa mumewe? Sipati picha.
 
Kaza apo apo hiyo ni difensive machanism kwa binti mwenye hamu sana na anajificha as if hahitaji lakini ana hamu kupitiza, rafik yangu aliwahi tukanwa mbaya sana tena mbele yangu hadharani lakini leo hii anamega hadi kinyaa na hataki kubanduka ingawa jamaa mpango nae. So bana apo apo usiache nafasi ata kidogo msaka cha uvunguni hiyo
 

Uambiwe mara ngapi bro? Itakuwa ulishapewa signs kwamba hakuhitaji but una force
 
Achananna watu ambao wameshavurugwa akili zao ambao hawako sawa, usikute huyo demu ni chizi tu aliwatu wanamuona yuko sawa

We cha umuhimu kaa naye mbali huu ndo ushauri wangu
 
Tupia kapicha basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…