Memtata
JF-Expert Member
- Jul 27, 2013
- 587
- 1,863
Ushawahi kusoma kisa changu cha mrembo Joyce? Sasa leo yananikuta sababu ya huruma yangu.
Joyce bana niliendeleza uhusiano nae, amenieleza shida zake nyingi na kujutia aliyowahi kuyafanya na kusema sasa anataka kutulia, mimi nikajifanya baba huruma nikamwambia usijali mama nitakusaidia kadri ya uwezo wangu. Kinachonikuta sasa nakumbuka semi hizi 'kunguru hafugiki' na 'sikio la kufa halisikii dawa' 😂
Ila wanaume huwa tuna huruma za ajabu na za kijinga. Unakutana na mwanamke humjui hakujui analia shida zake unajisemesha "nitakusaidia mama" 😢
Baada ya kukutana na Joy Kanda ya Ziwa na kunielezea kisa chake nikaingiwa huruma nikaamua kusimama kiume nikamwambia Joy mi nitakusaidia, kwanza ntakutafutia kazi angalau utoke mazingira haya ya bar na katika hili nikawasiliana na best yangu mmoja ambaye anafanya kazi kwenye kampuni inayohusika na chakula na usafi kwenye kampuni yetu. Akanambia wanatarajia kufungua kantini mpya kwenye location mpya so lazima waajiri watu wa kutosha. Nikamwambia Joy sio hili tu nitakusaidia kodi na kila kitu ili uanze maisha mapya, wakati huu Joy alikuwa anaishi ghetto la yule mdada mmiliki wa bar
Mungu si mimi, siku moja jamaa yangu akanipigia na kunipa taarifa kwamba ndani ya miezi mitatu wataajiri kwahiyo akaniomba nimtumie CV za Joyce. Dem hakuwa na chochote sababu aliacha shule akiwa kidato cha tatu! Kwa kuwa mimi mtoto wa mjini nikamtaarifu Joy alipokubali nikamuandalia kila kitu; o'level certificate, hotel management certificate na certificate of service nikamtumia jamaa + cover letter and resume. Baada ya kukamilisha hizi docs mkali akanambia inatakiwa subira tu ila mchongo ukikaa sawa lazima HR tumpoze kwa chochote, mwanaume nikasema hakuna shida nitasimamia kila kitu.
Wakati haya yanaendela mi nikawa naonana na Joy eneo lake la kazi lakini wakati huo huo something suspicious was happened. Joy ni mzuri kila mwanaume akimuona lazima ampende, kuna hawa vijana wa kufumania milioni leo na wanahakikisha iishe wameniumbua sana. Joy uvumilivu umemshinda 😂😂😂
Mapema baada ya kugundua hili nilimwambia Joy "mimi nimeoa na wewe umekuja hapa kutafuta maisha, kama unaona kuna kitu kina manufaa kwako usiniogope mi nitakuvumilia"
Joy kajifanya kwamba hawezi kunitenda maana mimi nimemsaidia sana, wakati huo kila siku hela ya kula na matumizi madogo madogo nilikuwa nampatia. Lakini haya niliongea kwa kumfurahisha Joy tu lakini ilikuwa kila nikimkuta Joy na mwanaume roho ilikuwa inauma 😂
Leo naandika haya nafikiri uvumilivu umefika mwisho, kuna jamaa yangu mmoja mshkaji kabisa niliwahi kuambiwa anatoka na Joy lakini Joy alikata katakata kila nilipomkuta au kumuuliza. Leo red handed nimeenda kazini kwa Joy bila taarifa nje nikakuta BM ya jamaa imepaki nje moyoni nikajisemea 'leo ni leo' 😂 naingia ndani namkuta kweli jamaa na wapambe wake kamkumbatia Joy! 😢. Najifanyaga sina wivu ila leo nimeumia sana.... Tatizo naumia kwa nani?! Joyce bar maid!!😂😂😂
Nikajikaza kiume nikasalimia kila mtu na kutoka meza za nje, Joy akanifata na kuniuliza 'mbona utatoka?' nikajibu shortcut 'niko sawa usijali'. Nikachukua embassy na kuondoka zangu 😂😂😂
Nilikuwa nimeacha pombe hapa nimeanza kunywa😂 nachojiuliza kwanini nashikwa kifala hivi na bar maid! Lakini najijibu labda ni sababu Joyce alinihakikishia kwamba ananipenda mimi tu. LAKINI NAJUA KABISA JOY ANAFANYA KAZI BAR!!!... kweli dem wa bar anipotezee muda!
"Muhudumu niongeze Heineken ya moto kama ulivyo!" 😂😂😂
Nilitaka tu kuelezea kisa hiki, hakuna haja ya maoni wala ushauri. Enjoy!! 😍