Huruma yetu ya machoni au machozi yetu tunayoyaonyesha hayawezi kubadili uamuzi wa mahakama

Huruma yetu ya machoni au machozi yetu tunayoyaonyesha hayawezi kubadili uamuzi wa mahakama

Rich Hash

Senior Member
Joined
Mar 7, 2017
Posts
149
Reaction score
203
Nilichokisema na ninachoendelea kukisema mpaka sasa ni kuwa, huruma yetu ya machoni au machozi yetu tunayoyaonyesha hayawezi kubadili uamuzi wa mahakama, kama tunadhani hilo linawezekana basi ni dhahiri kuwa ujinga huo umevuka kiwango cha kawaida.

Hiki kinachofanyika sasa mitandaoni ni sawa na kuipangia mahakama au kuiingilia, jambo ambalo kila siku tunalipinga. Kwa dhati kabisa nimpongeze wakili Jebra kwa kujitolea kuwasaidia hawa ndugu ktk kukata rufaa, hii ndiyo njia pekee na sahihi ya kuweza kupinga hukumu au kujiridhisha kuhusu hukumu ya awali na siyo vinginevyo.

Njia pekee ya kupambana na hilo ni kufuata utaratibu wa kisheria na kimahakama, na nilichokisema jana na bado nitaendelea kukisema ni kuwa wahusika washauriwe au wasaidiwe kukata rufaa iwapo wanazosababu zinazoweza kubatilisha hukumu ya awali.
Bila hivyo tutabaki kufanya maigizo na kutoa machozi ya huruma kwa kudhani huruma yetu inaweza kubadili uamuzi wa mahakama. Tusisahau kuwa, hatuwezi kuipangia mahakama wala kuiingilia ktk maamuzi yake.
Magoiga SN
1551018523793.png
 
Back
Top Bottom