Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Ninae huyu mtu anaeitwa Hussein Bashe, Kwa mlio karibu nae jaribuni kumuonya kwamba hicho kilimo anachojaribu kukianzisha, kimeshashindwa hata kabla hakijaanza .labda kwa sababu yeye ni mtu anaedhani kilimo kinaendeshwa kwa makaratasi, hivyo anajaribu kutoa mishipa ya shingo kwa kuongea sanaaa. Akijua ndio kilimo chenyewe.
Kwanza waliopewa nafasi hizo sio wakulima Kwa asili, ni vijana tu ambao wamesikia hekari zinagawiwa wamezikimbilia, ila vijana wenyewe wanaoishi kwa kilimo na wanailisha nchi tangia tupate uhuru hawajaguswa hata Mmoja. Kilimo hakiitaji makaratasi Bali asili ya mtu, kilimo ni asili usipokuwa nayo hata ukipewa zana zote hautaweza.
Na Rais amehadaika na hayo makaratasi ya Bashe anamwaga mamilioni ya pesa ambayo hata hivyo hayatakuwa na tija yoyote, nasema hayatakuwa na tija kwa sababu waliopelekwa sio wakulima ,wakulima hawajafikiwa na kilichofanyika ni kumlazimisha kuku wa kisasa akajitafutie chakura, nasema Tena mpango huu ungepelekwa kwa wakulima wanaozalisha mahindi Huko rukwa na ruvuma, kwa miaka yote wao wapo shambani hawategemei makaratasi, wao kilimo ndio maisha Yao.
Bashe anajaribu kutuingiza mjini kwa mradi huu ambao kufika 2025 hautakuwepo na hayo mashamba yatabaki mapori ya wanyama na hayawani. Kama mnataka Mali mtaipata shambani. Nendeni kwa wenye asili na kilimo mkawape sapoti ya kutosha mtaona matokeo lakini hii propaganda mnayojaribu kuileta hamtaweza mtakwama, narudia katika hili Nina uhakika mabilioni ya pesa yanaenda kupotea.