Hussein Machozi alizwa vitu vyake akiwa gesti - Singida (Stanley)

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
[h=3]HUSSEIN MACHOZI ALIZWA VITU VYAKE AKIWA GEST- SINGIDA[/h]


MKALI wa Bongo Fleva, Hussein Machozi amelizwa vitu vyake mbalimbali ikiwemo kompyuta mpakato ‘laptop’ katika gesti aliyokuwa amefikia iitwayo Stanley mjini Singida.
Chanzo chetu kilichoomba kuhifadhiwa kilisema tukio hilo lilitokea Ijumaa Machi 8, 2013 katika gesti hiyo ambapo staa huyo alikwenda kufanya shoo na alipomaliza alipitia kwenye kikao cha kupanga mikakati ya shoo nyingine iliyoandaliwa na Seif Shabani ‘Matonya’.

“Aliporudi sasa ndipo akakuta vitu vyake havipo na maelezo ya wahudumu yalikuwa yanamchanganya tu ndipo akaamua kwenda polisi. Cha kushangaza aliporudi alikamatwa na kuwekwa ndani kwa maelezo kuwa alifanya vurugu kwenye sehemu ya biashara,” kilieleza chanzo hicho.

Kikaongeza: “Mmiliki wa gesti hiyo aitwaye Halingumu ndiye aliyempeleka ndani.”

Akifafanua juu ya tukio hilo, Hussein Machozi alisema: “Ni kweli hilo tukio lilitokea. Laptop yangu yenye thamani ya milioni mbili ilipotea hivihivi kaka. Kilichoniuma zaidi ni mimi kwenda kushitaki halafu narudi nakamatwa na kugeuziwa kibao.

“Nililala ndani usiku mmoja, nikaachiwa Jumamosi asubuhi (Machi 9, 2013) kwa kusingiziwa kufanya vurugu na kujeruhi, kitu ambacho si kweli.”



 
hiyo nyumba ya kulala wageni ni moja ya nyumba maarufu sana singida ila inasifika kwa kwa mambo hayo.mmiliki wake ni mbabe sana na ye na polisi ni kama watoto waliochangia mama baba tofauti usitegemee haki hapo
 
Inasemekana guest maarufu ya Stanley ya mjini Singida ni maarufu kwa kuiba wateja wake ikiwa inamilikiwa na jamaa mmoja aitwaye Malingumu ambaye ni mbabe babe na anajuana na polisi wa pale Singida na inasadikiwa anahusika kwa namna moja au nyingine katika kuwaibia wateja wanaopanga hapo kwenye guest yake na kisha hata ukienda polisi hakuna chochote kitakachofanyika zaidi watakusingizia kesi nyingine

Hapa siko katika kumharibisa biashara jamaa la hasha ila niko katika kushtua wananchi, polisi, wakubwa wa polisi , wanaharakati katika kuichunguza hii guest na kumchukulia hatua mara moja huyu bwana Stanley...

MMOJA YA WAHANGA WALIOPATA SHIDA ZILIZOSABABISHWA NA HII GUEST BI MSANII WA BONGO FLEVA HUSSEIN MACHOZI KATIKA TUKIO LILILOTOKA HIVI KARIBUNI

SOMA MKASA MZIMA

 
Jina la Mmiliki wa Guest hiyo ni ujumbe tosha kwamba mahala hapo si salama. Anaitwa "Halingumu" usitegemee utamu wa asali ukatokea mdomoni mwa nyuki. Mdomoni mwa nyuki ni wimbo tu, patokapo utamu ndipo patokapo makali ya nyuki. HALI NGUMU NA MAISHA BORA ni mambo mawili tofauti.
 




Akhsanteni kwa taarifa ambayo ni muhimu sana kwangu maana naendaga sana kikazi Singida, kwa taarifa hiyo hata guest zote zikijaa sitaenda kulala katika guest hiyo wala kuulizia.
 
Duuu bora umenijulisha, nipo njiani naenda singida na hapo ndio nilikuwa nimepanga kukodi. Duu tena nina laptop 2 na digital camera 1, simu apple ya 1.2mil, asante ndugu kwa kunijulisha hayo majizi yanayofugwa na mipolisi. :crying:
 
Wengi tulikuwa tunatumia Hotel hiyo lakini kwa taarifa hizi sasa basi, Labda nifuate disco lao kama bado lipo..Sasa kwa wenyeji wa Singida ni Hotel ipi Nzuri angalau inayofanana na Stanley? Na je kile ki Guest House cha NBC kingali kinafanya kazi?
 
Na mwanza pk hotel ni pa kuogopwa kama ukoma ukienda na laptop au kitu chochote cha thamani utalizwa tu. Hotel iko karibu na furaisha barabara ya kwenda airport upande wa kushoto kama unaenda airport toka mjini.



 
Unajua siku wezi maboss wao ni polisi ndio maana wizi unakomaa sana, eti kisa polisi wanapokea mshahara mdogo. Hiyo guest ni ya kuchunguzwa haraka sana
 
Asante kwa kutujulisha huyo Malingumu atakuwa ni mtu hatari kwa kuwezeshwa na Polisi anaoshirikiana nao hapo Singida.
Hiyo Guest inayoitwa Stanley hapo Singida hawanipati kamwe bora nilale kwenye gari. Nikikosa kabisa pa kulala nitalala kwenye gari mahali penye walinzi na niwalipe hao walinzi ili wanilinde.
 
Utalalaje kwenye Guest house wakti hotel zipo? Siamini kama singida nzima hwana hotel
nyumba ikishaitwa Guest house si salam tena ....manake ni cha wote,
kwanza si salama 2,guest nyingi huwa ni wachafu wa kufua mashuka 3 ,hazina huduma nzuri kama maji + breakfast

unaweza ukakimbia ghalama ukajitia matatizoni
binafsi nazichukia hizi Guest hasa nikiwa safarini
 
singida 90% ya lodges and guest houses are not safe kabisa jamaa wa huku wana mioyo ya kikatili ajabu... Singida mjini giza likishaingia tu sio mahala salama hata kidodo
 
Sio guest house ni stanley motel 1992 ltd na pia ni mmiliki wa aqua vitae na travelers hotel karibu na stand mpya.
 
nitakua siendi pale kulala tena. Bora niendelee na gest zangu za elfu kumi
 
Wengi tulikuwa tunatumia Hotel hiyo lakini kwa taarifa hizi sasa basi, Labda nifuate disco lao kama bado lipo..Sasa kwa wenyeji wa Singida ni Hotel ipi Nzuri angalau inayofanana na Stanley? Na je kile ki Guest House cha NBC kingali kinafanya kazi?

Fikia guest za kanisa Katoliki, ni pazuri mno na wana vyumba vya bei mbalimbali na kwaajili ya watu wa makundi yote. Ulevi na Uzinzi hapo haviruhusiwi. Kazi kwako!
 
Sio guest house ni stanley motel 1992 ltd na pia ni mmiliki wa aqua vitae na travelers hotel karibu na stand mpya.

Sasa jamaa na mali zote hizi bado anahangaika na ukwapuaji wa vitu vya wateja.....duuhuh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…