Hussein Machozi: Mashabiki msimu ujao wataniona kupitia Soka, najiandaa kusajiliwa na Kagera Sugar

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,072
Hussein machozi katika pozi

Muimbaji wa Bongo fleva Hussein Rashid Dodi a.k.a Hussein Machozi, ametangaza kuwa mwakani (2016) huenda ukamuona akiingia uwanjani kuichezea timu ya soka ya Kagera Sugar katika Ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Akizungumza kupitia kipindi cha ‘Hatua Tatu' cha Times Fm, Machozi amesema kuwa kwa sasa yuko kwenye mazoezi makali kujiandaa kusajiliwa na timu hiyo.

"Nipo mazoezini sasa hivi kwa ajili ya kujiandaa na kusajiliwa na Kagera Sugar kwa ajili ya kuichezea msimu ujao, so mazoezi wanakuja wananitazama kila siku, kwa hiyo mashabiki watambue msimu ujao wataniona kupitia soka"Kabla ya kuanza safari yake ya muziki , kipaji cha kwanza cha staa wa ‘Kwaajili Yako' kilikuwa ni kucheza mpira.

Chanzo: Times FM
 
Isije kuwa ya Kajumulo kulazimisha kucheza mpira wakati hawezi.
 
Husseini machozi ccm walimtumia kama toilet paper mpaka akapotea kimuziki kama amejipanga kwenda kwenye mpira ni jambo jema .
 
Mpira anaujua tatizo ubishoo!! Nilimshangaa sana alipochagua kubana pua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…