Zanzibar 2020 Hussein Mwinyi bora ukawaachia - Ombi la wazi

Zanzibar 2020 Hussein Mwinyi bora ukawaachia - Ombi la wazi

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Kwa maoni mujarabu kabisa ni bora Nd. Hussein Mwinyi akawaachia ugombezi wa Uraisi wa Zanzibar kwa maana ya kujitoa hii itakuwa fahari yake milele kwani kufanya hivyo ni kuiepusha Zanzibar na shari na dhiki zinazoinyemelea.

Kama Muislamu Mkereketwa hakuna haja ya kuzozana heshima atakayoipata ni zaidi ya yeye kuwepo ndani ya CCM,sisemi kwa kuona hafai kuwa kiongozi la hasha ,anafaa tena anafaa sana ila upepo unaovuma sio wa kutweka.

Yeye kama mpembuzi ameshalijua na asikubali kufanywa chambo cha mauaji ya Waislamu yanayotayarishwa na watu wale ambao tumewasikia wakikusudia kupiga kambi katika visiwa vya Zanzibar, huko hawaendi kuuliwa wapinzani wanakwenda kuuliwa Waislamu maana kinachosemwa sasa si kupiga kura ni kuilinda Zanzibar kama nchi na wananchi wake,

CCM wengi waliokuwa mstari wa mbele wamejitenga na Hussein Mwinyi hili halina shaka,tunasikia ya watu kuondoka anapoingia Hussein Mwinyi, hili halisaidii uislamu bali hubomoa na kutufanya tuonekane watu wa ajabu sana.

Nimjuavyo Hussein ni mtu wa dini sana tofauti na maraisi wote waliowahi kupita kwa nimuonavyo, sijui ndani ya moyo wake,rai yangu ni kujiengua na ALLAH atamlipa kubwa zaidi kuliko uraisi wa Zanzibar.
 
Zanzibar ni nchi ya kifalme... familia tu zinarithishana uongozi... akitoka mwinyi inakuja zamu ya mtoto wa shein ama salmini kisha karume tena
 
1599448043233.png
 
CCM waislam
WApinzani Waislam
Kwa nini usiseme kuwa Uchaguzi uwe wa haki? Mshindi wa kweli atangazwe
 
Hussein Mwinyi ni mtu sahihi kwa maendeleo ya Wazanzibari.
 
Nilimsikia Dr Hussein Mwinyi baada ya kuteuliwa kugombea u-Rais Zanzibar alisema "Nitakuwa mkali kama Magufuli".

Hapo ndipo alipoharibu na kushindwa kabla kampeni hazijaanza
 
Kama Muislam Mkereketwa?
Acha udini!
 
Back
Top Bottom