Hussein Siyovelwa Atembelea Maktaba

Hussein Siyovelwa Atembelea Maktaba

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
HUSSEIN SIYOVELWA ATEMBELEA MAKTABA

Leo Maktaba imetembelewa na Hussein Siyovelwa mtoto wa Peter Said Siyovelwa mmoja wa wapigania uhuru wa Tanganyika.

Hussein ameandika miswada miwili ambayo inasubiri kuchapwa kuwa vitabu.

Hussein ni mzungumzaji mzuri na ana mengi aliyochota kutoka kwa marehemu Mzee Siyovelwa.

Kwa zaidi ya saa moja nilikaa wima nikimsikiliza akinihadithia mengi katika tasnia ya uandishi kwani yeye kafanya kazi katika magazeti mengi.

Halikadhalika alinigusia mkasa uliomfika baba yake wakati wa utawala wa Rais Nyerere uliosababisha Mzee Siyovelwa kujiuzulu wadhifa wake na akafuatiwa na Ali Hassan Mwinyi.

Hussein Siyovelwa alinisisitizia kuwa baba yake ndiye alijiuzulu kwanza kabla ya Ali Hassan Mwinyi.

Huwezi kuchoka kumsikiliza.

Hii ni sehemu ya kwanza ya mazungumzo yetu:


View: https://youtu.be/8STn7z4cd7Y?si=D02DtrWc8-ZqMDdF
 
Back
Top Bottom