Hussein Yamodo ni shujaa asiyeimbwa.

Hussein Yamodo ni shujaa asiyeimbwa.

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Posts
23,372
Reaction score
54,943
Huwenda asijulikane kwa wengi kutokana na muziki anaofanya kupendwa na idadi ndogo ya watu ila kipaji halisi cha muziki kiko ndani yake.

Yamodo ni mwanamuziki wa dansi, kwangu mimi nilianza kumsikia mwaka 2015 kwenye wimbo wake wa "Nimezaliwa pekee yangu" hakika kwa mtu wa muziki mzuri hawezi kushindwa kukubali kipaji cha kijana huyu. Ni mara chache sana mchango wa mtu kama Yamodo kuonekana kwenye tasnia ya muziki hasa kwa zama hizi ambazo upepo wa muziki umebadilika na dansi kuhamia kwenye kumbi za starehe.

Heko kwako Yamodo acha nikupe sifa zako kabla hujafumba macho au mimi sijafumba macho.

Baadhi ya nyimbo ambazo kaimba Yamodo ni pamoja na: Penzi la Dhoruba, Moyo wa huruma na nyingine nyingi.

images.jpeg
 
Mnao mchokonoa mtoa mada labda hamumjui.. ngoja aje awape majibu yake hadi mkimbie jf
 
Yamodo huyu jamaa namkubali sana, nakumbuka kuna kipindi alikuwa dodoma anapiga show zake kule. Kama bado yupo mikoani namshauri aende dar akajichanganye huko nafikiri ndio anakoweza kuonekana zaidi
 
Naam! Makazi yake yalikuwa Dodoma. Nadhani unaona kipaji chake kilivyo juu.
Yamodo huyu jamaa namkubali sana, nakumbuka kuna kipindi alikuwa dodoma anapiga show zake kule. Kama bado yupo mikoani namshauri aende dar akajichanganye huko nafikiri ndio anakoweza kuonekana zaidi
 
Back
Top Bottom