"Hutopata mwanamke atakayekupenda kama mimi."

kalou

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2009
Posts
4,975
Reaction score
3,829
Kwa wanaume ambao wameshakuwa na mahusiano at least zaidi ya matatu watakuwa mashuhuda wangu hapa sababu najua kwenye hizo break ups lazima utakuwa umeshawah kukutana na haya maneno!."hutapata mwanamke atakayekupenda kama mimi"..na mara nyingi baada ya kuambiwa haya maneno hufuata matendo yaliyo kinyume kabisa,kama mwanamke kutaka kulipiza kisasi na vitisho vingine..
serioulsy wadada huwa mna maanisha nini mkisemaga hivyo coz najua wengi humu mlishajikuta kwenye situation mkasema HUTOPATA MWANAMKE ATAKAYEKUPENDA KAMA MIMI.!
 
Ngoja nijifiche pale ningoje waje!
 
Mfa maji hakosi kutapatapa. Kwani anajua nilikotoka nimesha kutana na wangapi ambao wananipenda zaidi yake..? Mi nafikiri hizo ni kauli za kushindwa tu, hazina mantiki..
 
Kaka halafu wanawake wanaosema hivi huwa wazuri lakini vichecheeeee....vinapasua kichwa ile mbaya.
 
Kaka halafu wanawake wanaosema hivi huwa wazuri lakini vichecheeeee....vinapasua kichwa ile mbaya.

true dat,kidizaini una give up afu ukimwambia anaanza hayo mambo
 
Bora wao wanaosema hivyo, lakini wanaume lazima kitanuka.......... Kuna mwanaume anayeachwa na mwanamke akae hivi hivi bila kutia neno..! Lazima vitisho na kejeli vitatawala, kama ataamua kukaa kimya basi atakuwa ananung'unika kichini chini, kwani lazima atakuwa ameumizwa............
Hii ipo kote kote wakuu.

 
hiyo kauli nimewahipewa na my ex miaka 4 iliyopita ila ndio ivo upepo tu maana kwa sasa nina GF mzuri na maisha yanasonga na upendo ni zaidi yake hata nashangaa muda ambao nilipoteza nae.
 
 

Asilimia kubwa ya wadada/wamama wanaamini hakuna aliebora kumzidi yeye. na hiyo ndio kasumba ya wamama wengi. Na kwa utafiti usio rasmi unaonyesha kuwa migogoro mingi inayotokea kati ya kina mama mkwe na wake za vijana wao husababshwa na kasumba hiyo. Mama anaamini kuwa mke wa kijana wake sio bora kama alivo yeye kwa baba.
 
 
Bora kauli hiyo kuliko vitisho vya wanaume mwenyewe utaogopa hata kutoka ndani
 
Mimi nishakutana na hiyo kauli sana tuu kauli ingine ni hii "Hutopata mwanamke mvumilivu kama mimi"
 
Sijawahi huwa nakaa kimya anarudi mwenyewe eti oh kote nilikoenda hakua kama wewe nipe nafasi sjui utajona upo eden.hahhahaha raha kweli mtu akijirudi halafu ndo humtaki tena
 
Sijawahi huwa nakaa kimya anarudi mwenyewe eti oh kote nilikoenda hakua kama wewe nipe nafasi sjui utajona upo eden.hahhahaha raha kweli mtu akijirudi halafu ndo humtaki tena

wamesha rudi wangapi kwako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…