Huu kweli ni utoto aisee

Drjacka92

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2016
Posts
445
Reaction score
522
Habari Ndug!.
Kiukweli nimekumbuka zamani sana Leo, kuna mambo ambayo nilivyokuwa mtoto mdogo niliyadhania tofauti nauhalisia wake kwakwelii. Mfano wa mambo hayo ni
1.Nilidhania kuwa Daktari huwa haugui.
2.Nilidhani kuwa Padri, huishi milele bila kufa
Hayo ni baadhi tu, nawewe kama kuna mambo uliyafikiri tofauti enzi zautoto unaweza kuongezea Ili tujikumbushe utoto wetu.

Amani kwenu!.
 
Nilikuwa nafanya nao ule mchezo wa baba na mama siku nilipotahiriwa nikawa sifanyi tena eti naogopa watazaa na wao vilele walikuwa wananiogopa baada ya kutahiriwa[emoji86] [emoji86]
 
Mi nilifdhani wakubwa uwa hawanyi (hawajisaidii)haswa haja kubwa, na condom tulizokuwa twaona barabarani tulidhani ni maputo ya wahindi
 
Nilipokua mdogo sikuamini kama mama au baba yangu kuna siku anakosa pesa ya kunipa ninapoihitaji, mara zote nilipojibiwa na mama/baba kua mwanangu sina pesa nilikasirika nikajua wanakataa tu pesa wanayo
 
Nlijua tanzania ndo nchi tajir kuliko zote duniani ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…