Nikiangalia shilingi, naona ipo vile vile na kama tofauti ipo basi ni ndogo sana...
Kama ndivyo, jiulize kilichopo ni Cost-Push Inflation inayosababishwa na kupanda kwa gharama za uzalishaji au ni Demand-Pull Inflation inayosababishwa na kuongezeka kwa demand ya bidhaa?!
Hata kama ukusanyaji data ni muhimu lakini sidhani kama hapo napo nalazimika kuingia field kufanya research kama ni Cost-Push or Demand-Pull Inflation coz' dalili zote zinaonesha ni Cost-Push Inflation, ambayo si kwamba inatokana na factors zingine kama vile kuongezeka kwa mishahara as w ell as other fiscal policies, bali:-
1. Bei ya mafuta soko la dunia imepanda,
2. Tukaongeza tozo kwenye bei ya mafuta ambayo tayari yamepanda!
Matokeo yake: Bei ya Juu ya Mafuta Soko la Dunia + Tozo za Juu kwenye Mafuta nchini = Bei ya Juu ya Mafuta Nchini!!
Kila mmoja anafahamu mafuta ni nini katika uzalishaji!! Sasa kama uzalishaji wetu unategemea mafuta, ina maana automatically Gharama za Uzalishaji Zitapanda... tunarudi hapo juu kwenye Cost Push Inflation!