Huu Mgao wa Umeme shida ni nini?

Mr. Wise

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2012
Posts
7,733
Reaction score
6,469
Habari za majukumu!
Kuna mgao unaendelea hapa Arusha, Umeme unakatwa asubuhi unarudi saa moja kasoro usiku. Tanesco kwanini wasituambie shida ni nini?
Mlituaminisha mgao uliopita ni sababu ya kufanya maintenance, ni juzi tu mkatangaza maintenances zimeisha sasa hii ni nini?Nadhani kuna mahali hapako sawa sasa, maana hatuelewi nini tatizo.

Nimewasilisha.
 
HaTa Mwanza ni mgao kila kukicha
 
Tanesco hawashindwi kusema mgao unasababishwa na vita ya Ukraine, ngoj tuwasubiri hapa tuwasikie
 
tulia mkuu, si uliambiwa kipindi cha JPM motambo haikufanyiwa marekebisho au umesahau
 
Jamaa amefeli sana kuongoza hii wizara na wanavyompamba chawa wake mitandaoni, inachosha hata kama dharau kwa wananchi sio kiivyo, kodi zetu ndio zinawafanya waishi vizuri na umeme tunautegemea kwa kazi nyingi
 
Kila sehemu ya nchi
 
Huyu waziri ni mtu asiye na maana, siyo mzalendo kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…