Huu mkataba unambana mpangaji na kumbeba mwenye nyumba

Kaweka ndogo sana alitakiwa kuweka laki 5 kwenda juu. Mi nyumba zangu zote ni milion ela ya maintenance mzee
 
Hiyo itakufanya uwe makini na nyumba ya watu
Mpangaj anatoka kwenye chumba kipo kama Kuta zile zinazchorwa rangi barabaran mitobo Kila Kona Hadi milangoni ukiingia choon hasugui Kuta za pemben tiles yaan kama choo Cha stand
Huyo mwenye nyumba kajiongeza ila iyo hela inalipwa mpangaji anapoingia au katikati?
 
Kajenge uhamie kwako.
Hapo hajaweka sharti la kwichikwichi hataki kusikia unalalamika
 
Wenye nyumba wanazingua sana,yaani hata matatizo ya umeme yakitokea kwenye nyumba yake iliyosababishwa na miuondombinu yake mibovu basi analipishwa mpangaji.
 
Nyie wapangaji ni waharibifu sana wa nyumba.hasa nyie mnaolipa elf 50 kwa mwezi kama kodi
 
mikataba ya nyumba/vyumba uswhailini ipo kwa ajili ya kumbana mpangaji tu. mimi niliambiwa mwisho kuingia ndani saa 4, na pia hakutakiwa wageni wa mara kwa mara
 
Security deposit, inatakiwa iwe kodi ya mwezi mmoja na endapo hakuna uharibifu uliofanyika katika nyumba wakati wa kuhama, itarudishwa yote. Kama kuna uharibufu, utashirikiana na mwenye nyumba kufanya marekebisho kisha utarudishiwa kiasi kitakachosalia. Kama security deposit haitoshi utaongeza ili kuondoa uharibufu ulioufanya😀
 
Hicho kiwango kidogo sana ilifaa ianzie 200,000 kwenda juu
 
Mjitahidi kusoma vitu kwa umakini "Kama hakuna uharibifu unarejeshewa pesa yako"
Sema changamoto yake,
Itasababisha uharibifu WA kukomoana Kwa wapangaji (WASIO wastaarabu) pindi wanapohama.
 
Kitaalamu hiyo inaitwa "Key Deposit"
 
Anapoingia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…