TFF ni shirikisho la mpira wa miguu linaloendeshwa kihuni sana, wale jamaa pale Karume wanajiona miungu watu.
Huo mkataba wa TFF na GSM lazima una contents za hovyo ndio maana unafichwa, ni ujinga wa hali ya juu sana kutishia watu kuwashtaki endapo wataujadili, hili sio taifa la mazezeta kama wanavyodhani wale wahuni.
Katiba yetu inatoa uhuru wa kutoa maoni bila kutuwekea mipaka, wao TFF na GSM wanakuja na kamkataba chao cha kihuni kutuzuia tusiujadili, ni wapuuzi sana wale jamaa, corrupt leaders, na ndio wanajidai wamefunga... nonsense.
Nitashangaa sana kama timu za mpira wa miguu ligi kuu vitanyamaza kimya kama walivyotishwa na hao wahuni, wao ni shareholders wana haki ya kujua chochote kinachohusu mpira wao, sheria zote za nchi hii ziko upande wao, wasiwe wajinga wakanyamaza kimya.