Huu Msemo Chanzo/Asili yake ni Nini?

Huu Msemo Chanzo/Asili yake ni Nini?

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,265
Huu msemo unatumika sana pale mtu anapotaka kuweka taswira ya kuponda raha/maisha kwa kusema 'anakula bata'.
Je, katika utamaduni wetu sisi watanzania bata ana nafasi gani? Kwa nini haikuwa kuku? =Mwenzetu kafanikiwa sana, anakula kuku tu. Au hata mbuzi = Yuko majuu bwana, anatafuna mbuzi.

Nauliza: Kwa nini bata? Tena kwenye huo msemo wanaongeza neno mrija. = 'Anakula bata kwa mrija' Bata ni nyama au kinywaji?

Naomba msaada wadau wa lugha juu ya huo msemo.
 
Mkuu neno bata lilitokea huko temeke mikoroshini na limetumika sana kwenye nyimbo zao wakimaanisha kuvuta bangi nadhani watu wamekuja kulitohoa na kuwa kula raha ilo la kula kuku linatumika sana kula kuku maana yake ni kupumzika kwa kutokufanya kazi ya kila siku lakini ni kwa mda kwa kishule ni kutokwenda prepo/kutopiga msuli kwa siku hiyo.

kalale upitwe kama umesimama(kuku)
 
Mtoa mada swali kwako,
Kwani Raha inapondwa
Unajua Kuponda?


Hebu jibu kwanza na mm ntapata cha kuchangia.
 
Kula kuku kwa mrija lilikuja enzi za nyerere ambapo kula kuku kwa umma na kisu na juice kwa mrija vilikuwa vitu nadra kwa wananchi wa kawaida....sasa mwisho watu wakawa wanaongea kinyume as kutania..wakawa Wanasema kuku kwa mrija juice kwa umma....so ndo asili yake huko..
 
Mtoa mada swali kwako,
Kwani Raha inapondwa
Unajua Kuponda?


Hebu jibu kwanza na mm ntapata cha kuchangia.
1gb Upo msemo 'Ponda raha kufa kwaja'
Umeshausikia au bado?
 
Last edited by a moderator:
Msemo Mtambuka "kula Bata " umetumia nomino mahsusi kwa kuwa Bata kiasili ni Ndege ambae sana hupenda raha ; mara nyingi Hali hii hudhihirika pale ambapo... Hushinda kwenye majimaji na kuogelea.... Hali hii ya kimazoea au maana ya kifasihi humjenga mponda raha kama anakula Bata... Kwa kusharabu maisha ya Bata... Ndio maana Fasihi ya Kiyunani au Biblia Takatifu inamchora mnyama mjanja kuliko wote wakati Huo ni Nyoka badala ya Sungura kwa Afrika Mashariki
 
Back
Top Bottom