Huu msemo unatumika sana pale mtu anapotaka kuweka taswira ya kuponda raha/maisha kwa kusema 'anakula bata'.
Je, katika utamaduni wetu sisi watanzania bata ana nafasi gani? Kwa nini haikuwa kuku? =Mwenzetu kafanikiwa sana, anakula kuku tu. Au hata mbuzi = Yuko majuu bwana, anatafuna mbuzi.
Nauliza: Kwa nini bata? Tena kwenye huo msemo wanaongeza neno mrija. = 'Anakula bata kwa mrija' Bata ni nyama au kinywaji?
Naomba msaada wadau wa lugha juu ya huo msemo.