Huu msemo wa "hatuna teknolojia" una maana gani?

Huu msemo wa "hatuna teknolojia" una maana gani?

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Habari wakuu,

Kuna msemo umezoeleka kwa Mambo fulani kwamba tunataka kutekeleza jambo fulani lakini hatuna teknolojia ya kuwezesha jambo hilo kufanyika.

Mfano raslimali yetu ya madini tunataks kuichimba wenyewe lakini hatuna teknolojia hiyo. Huwa najiuliza swali: teknolojia ni kitu mtu alipewa na mtu fulani au roho fulani au teknolojia ni zao la akili ya binadamu?

Mimi naamini bila shaka historia pia inakubaliana nami kwamba mwanadamu akitumia akili yake kwa bidii anaweza kufikia maendeleo makubwa katika teknolojia. Huu uvivu wa kusugua vichwa vyetu kuweza hata kutengeneza Simu ya mkononi aka Simu ya tochi unatugharimu.

Tunaishi kwa kutegemea wengine wafikiri na kubuni kwa niaba yetu. Tuna wasomi chungu nzima lakini mabingwa wa nadharia tu. Kwenye vitendo hawatusaidii lolote. Wana vyeo vya kitaalum tu, B.Sc, B.Eng, M.Sc na kadhalika lakini hawabuni nyenzo za maana kulisaidia taifa.
 
Rudisheni kwanza pesa za utalii, ndege na matengenezo hewa!
#vikaoomillion600
 
Back
Top Bottom