Huu mtandao wa utekaji watoto unaratibiwa na nani na kwa faida gani?

Huu mtandao wa utekaji watoto unaratibiwa na nani na kwa faida gani?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Utekaji na kupotea kwa watoto kunakotokea kwa sasa kuna viashiria vya mikakati ya kundi la watu wenye nia ya kuondoa utawala fulani madarakani.

Hali kama hii mara nyingi umalizika kwa kuondolewa waziri au IGP ofisini. Si kwa sababu siyo wachapa kazi bali ni kurejesha imani ya dola kama wanavyojiuzulu wanausalama wengine Duniani.

Kwa maoni yako nini IGP na Waziri wa Mambo ya ndani wafanye kukwepa shinikizo la watekaji? Wananchi wanapoendelea kusindikiza watoto wao shule na kuripoti case kila siku amani itakuwepo?

Leo inasambaa clip ya mtoto mdogo wa miaka 16 aliyekamatwa akiteka mtoto na anadai tayari mtoto mwingine ameshapelekwa kwa kiongozi wao. Je wananchi wanaweza kuamini huyo anayewatuma ni mtu wa kawaida asiye na connections?

Lengo la watekaji ni nn?
 
Lengo la watekaji ni nn?
Lengo la mtandao wa utekaji ni moja tu "Kuleta taharuki kwa wananchi waichukie mamlaka". Mengi yamefanyika huko nyuma lakini hayakufanikiwa (Mgao wa umeme, Sukari, panya road).

Siamini hata kidogo kuwa mtandao wa utekaji una nia ya kibiashara. Kwani kama ungekuwa wa kibiashara, ungeibuka ktk mikoa mingi na usingekuwa na speed ya mwendo kasi hii. Mengi yatajitokeza mpaka 2025.

La msingi ni kwa mamlaka kutoyapuuzia na kuutafuta mtandao huo na kuudhoofisha.
 
Mmewakaribisha waarabu Bandarini je huwa mnajua kafara zao? Tulieni hivyohivyo mtapata tu Akili ila kubwa ondoeni takataka za visiwani huku Tanganyika
 
Jambo jema kuna watekaji wameanza kukamatwa, mtandao utajulikana au umejulikana.
 
Huku kijijini wamama wanapagawa, watoto wenyewe hawajui kutulia, yaani amani haipo, watoto hata masomo ya jioni huko shuleni hawaendi tena.

Wakati mwingine unashindwa kujua hata unawaza nini 😙😷
 
Mmewakaribisha waarabu Bandarini je huwa mnajua kafara zao? Tulieni hivyohivyo mtapata tu Akili ila kubwa ondoeni takataka za visiwani huku Tanganyika
Huu ni uoga usio na msingi. Msitutoe kwenye reli. Waarabu wamejaa Marekani, Uingereza (Man City, Newcastel n.k), Ufaransa (PSG, Peugeot n.k), Ujerumani n.k. Yaani hapa TZ kwa hao wachache tu ndio iwe kelele.

Tumekopa (benki ya dunia) kujenga Mwendo kasi, mpaka leo haujalipa hata senti tano kwenye deni husika, kisa wazawa. Mtanzania anataka huduma na pesa ilipwe toka ktk mradi si kodi ya kukusanya K-Koo.

Mi sajali kama ni mchina, Mzungu, Dangonte, Muarabu, n.k. Tunahitaji huduma.
 
Back
Top Bottom