Huu mti una uhusiano na jina Ilala na Mikocheni?

Huu mti una uhusiano na jina Ilala na Mikocheni?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Kuna mkuu humu jana ameniambia kuwa huu mti(Palm) kwa kiswahili unaitwa Mkoche(Kisayansi Hyphaene Coriacea) Unapatikana pwani ya Afrika Mashariki kutoka Somalia hadi South Afrika na Namibia. Huko kusini ya Afrika unajulikana zaidi kama Ilala.

Kuna uwezekano mkubwa jina Mikocheni limetokana na uwepo wa miti hii eneo hilo.

Kijerumani mmea huu unaitwa Ilala pia. Kuna uwezekano mkubwa Wajerumani walilipata jina hili walipokuwa huko Namibia. Walipofika Dar na kuikuta miti hiyo wakapaita mahali hapo Ilala.

BTW: Mmea huu unavutia sana na una matunda(Makoche) yanayoliwa.

1717500329714.jpeg

1717500373714.jpeg

1717500401753.jpeg
 
Ilala lilitokana na maeneo hayo kuwa na waislamu wengi wa wenye kufuata toba ya allah hivo wenyeji wakapaita maeneo ya Lailah hailalah.Watu wakashindwa kutamka wakaishia ilala ! Na hata eneo la amana pale kulikuwa na benki ya kuweka pesa au amana zao na ndo mpaka leo panaitwa amana !
 
Back
Top Bottom