Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kuna vitu vinashangaza mnoo katika siasa za CCM ambapo kile kinachoimbwa majukwaani (kuwawezesha vijana na wanawake) ni tofauti kabisa na kile kinachofanyika. Hili la wazee wastaafu waliochoka na kuchokwa kurejeshwa kinguvu kwenye ulingo wa kisiasa ni miongoni mwa maajabu ya siasa za CCM.
Hizi harakati hazikuanza leo wala jana, tangu John Malecela akiwa mzee mstaafu (amekalichwa benchi) na kuanza kulala usingizi, ghafla miaka ya mwanzoni 2000 Mkapa akamkurupusha toka usingizini na akampa umakamu mwenyekiti wa CCM, alichokifanya Melecella ni kutengeneza mtandao wake wa kisiasa na 2005 akakamata fomu yake ya kutaka kugombea urais bahati mbaya 'wahuni' wakamkata juu kwa juu kwa fitna!
Magufuli naye akamteua mzee mstaafu aliyechoka, mzee Mangula akiwa amestaafu, yuko zake shambani akilima Nyanya zake, maisha yamemchapa kweli kweli akaokota dodo, akateuliwa kuwa makamu mwenyekiti, katikati ya harakati akalichwa sumu akiwa Lumumba, mzee wa watu chupu chupu akaponea Muhimbili.
Samia akarudia hayo hayo kwa kumteua mzee mstaafu aliyechoka, mzee Kinana kuwa makamu mwenyeki, Kinana naye 'akachonga ule mtego' aliposhtukiwa akakatwa juu kwa juu na ili kuficha yaliyo nyuma ya pazia akaigiza kutema bungo , na leo Samia amerejea tena kumteua Wassira, baada ya muda yatakuwa yale yale tu. Mzee Wasira tunajua, na hajawahi kubadilika.