Huu ndio mkataba wa Karl Peters na Chifu Mangungo ulitufanya tunawekwa chini ya Mjerumani

Huyu Mangungo kaburi lake liko wp!?
Hakuna anayefahamu lilipo kaburi wala mahali alipoishi Chief Mangungo.Wakazi wa Kijiji cha Msovero pamoja na serikali ya hapo Msovero wote hawana taarifa za Chief Mangungo wala akaburi lake.Wengine wanasema huenda baada ya kusaidi mkataba na ndugu yetu Karl Peters basi huyu chief alihamishwa.

Uchunguzi pia unaonyesha kuwa hapo Msovero kuna watu wanaitwa Mahungo na kabila lao ni wakaguru.Inasadikiwa kuwa wazungu walishindwa kutamka Mahungo na kumuita Mangungo.Inasemekana huu ukoo wa Mahungo hapo Msovero ni watoto wa Chief Mangungo.
 
Utata historia ya Chifu Mangungo
 
Uwongo, huo mkataba alisaini vipi wakati hajui hata kusoma? Uko wapi huo mkataba tuoneshe picha
 
Hivi unadhani hata angekataa kusaini huo Mkataba ardhi isingechukuliwa ?, Hizo ndio zinaitwa a deal you can't refuse...,you are damned if you do and damned if you don't...

Pili huo Mkataba haukuwa kwa manufaa ya Huku kwetu ni kwa manufaa yao wenyewe kuona nani achukue nini..., isingekuwa mjerumani, basi mfaransa / mreno au muingereza... kwenye hii equation mbantu has no say...
 
Zitto Zubeir Kabwe
 
Yaani ilitakiwa makaburi yafukuliwe wachomwe moto
 
WELL SAID!!! Wewe jamaa una maarifa sana.
Wengi wanamponda Chief Mangungo sababu hakwenda shule kujifunza ELIMU YA WAZUNGU (education) hii ambayo sie Kizazi hiki tumepata bahati ya kujifunza.
ILA KWA KIPINDI KILE HUWEZI KUMLAUMU CHIEF KIVILE SABABU ELIMU YA WAZUNGU KWA SIE WAAFRIKA ILIKUWA BADO HATUIJUI.
WATU TUNASAHAU KUWA HAYA MAARIFA TULIYONAYO SASA YA ELIMU, NI MATOKEO ELIMU TULIYOJIFUNZA KUTOKA KWAO WAZUNGU. Hivo tusijione wajanja sana kuliko Chief Mangungo. Kisa tu tumejifunza Kusoma, Kuandika na Elimu nyingne za Wazungu (Formal Education).
AFU KIPINDI HIKO HAKUNA SHULE (Formal Education) na Hakuna RADIO, TV, SIMU, UMEME wala INTERNET... Wala hakukuwa na MAGARI pia wala Barabara za LAMI!! Sasa unadhani Chief Mangungo angepata wapi maujanja kama haya tunayoyapata katika kizazi hiki??
CHIEF MANGUNGO HATA KAMA ASINGESAINI BADO ARDHI INGECHUKULIWA TU APENDE ASIPENDE. #Fact #Fact
 
Kwa kipindi hiki Chifu Mangungo na wenzake kama wangekataa ingekuwa na athari kubwa kwa Bwana Karl Peters.

Karl Peters alikuwa mtu mahiri na mwenye maono. Hakuwa na chochote zaidi ya kampuni yake na dhamira ya kutengeneza makoloni kwa ajili ya nchi yake.

Alicho kimudu vyema bwana Dr. Peters ilikuwa ni "The art of leveraging". Chiefdoms zilikuwa ni mwiba Kama zingekataa, Sultan wa Zanzibar naye alikuwa mwiba kwake..

Dr. Peters alichotaka ni kupata ushahidi kwa serikali yake kuwa wazawa wamekwisha kukubali kutawaliwa bila vikwazo, kwa Sultan hii imemaliza ugomvi kama atataka kupigana kuwarejesha wazawa kwake ..Dr. angepeleka mikataba Ujerumani ili nchi yake itume msaada wa kiulinzi na kifedha.. na ndicho kilichotokea.

Nina imani kama wangekataa wazawa, akina Mangungo Ujerumani isingekubali kumpa ufadhili Dr. Peters na huenda angeendelea mbele kutafuta makoloni mengine.

Mangungo alituangusha. Au petters alighushi mikataba hii.. maana he was too ambitious.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app

KeyserSoze
Benzodiazepine
 
Yeah nakubaliana na wewe.
ila Bila hao wakoloni pia nchi za kiaAfrica zingekuwa ni vinchi vidogo vidogo viiiiiiiiiiingi. Hizo chiefdoms ndo zingekuwa nchi mpaka sasa.
Hili Li-Tanzania loooooote kubwa lisingekuwa nchi moja. Probably Mimi na wewe Leo tungekuwa nchi mbili tofauti.
Maana Hio Mipaka ya Kuunganisha Chiefdoms na kusema hii iwe Tanganyika, hii iwe Ghana, hii iwe Gabon etc. yote hii mipaka ni wao.
Na wamesaidia zile Chiefdoms zikawa na Umoja ili kumtoa common enemy (mkoloni).
Yeah Mangungo alituangusha ndiyo, lakini vyovyote tu vile bado chiefdom ya Msowero ingetawaliwa tu due to lack of unity na poor technology.
 
Mkwawa,na Mangi meri walikuwa wanajua kusoma na kuandika kiarabu.Suala ka uelewa wa baadhi ya machifu ilikuwa si haba.Inawezekana Mangungo alitishiwa kuuwawa na wazungu.Yaani utoe ardhi yako halafu wewe uende kuishi wapi hasa kipindi hicho wanategemea ardhi mito na misitu.Naona hamuutafakari vizuri huo mkataba.
 
Mkuu hizi tawala zingekua. Kabisa.

Wenye nguvu wangewatawala wengine na serikali za mseto zingundwa na mataifa yenye nguvu yangeumbika.

Sema yangekuwa na utamaduni tofauti na.mifumo ya maisha tofauti kabisa. Ni dhana potofu kuamini vinginevyo..

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Eth Etheopia ni mojawapo ya nchi ambayo haikutawaliwa na mzungu.Waitaliano walijaribu kuivamia walikiona cha moto.Etheopia walikuwa wakimiliki gun kama wazungu,waitalia waliamua kuahirisha.Maendeleo yaliopo Etheopia hatuna tofauti na sisi, ikumbukwe Etheopia ilikuwa empire kubwa sana zama za kale
 
Bagamoyo port Iko njiani,

Tunakwenda kuuzwa.
 
Mkataba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…