Huu ndio mkataba wa Karl Peters na Chifu Mangungo ulitufanya tunawekwa chini ya Mjerumani

Kwahiyo Ramzan wa mkataba wetu ni nani sasa hivi?
 
Kwenye Bible kuna mtu anaitwa Jezebel. Alikuwa mke wa mfalme Ahab. Alisababisha matatizo makubwa kwenye utawala wa Ahab. Ni story ndefu kidogo. Baadae alikufa. Cha ajabu baada ya miaka mingi. Kanisa linakemewa ktk kitabu cha Ufunuo kwamba yafaa wamkatae Yezebeli maana bado yupo kwa namna nyingine. Nataka kusema nini. Akina Carl Peter, Ramazan na akina Mangungo huweza kurudi ktk roho ileile ila miili tofauti.
 
Mangungo naye alikuwa kilaza, hakushanga Karl Peters amekuja lini na mkalimani wake sijui Mluguru, Mkaguru nk. amejua Kijerumani lini!
 
Mkataba haukuwa kwa Faida ya Waafrika wala Waafrika walikuwa hawana Say Mkataba huo ulikuwa ni kwa ajili ya wao Waliosign mkataba kama kinga ya wengine wataokuja baada yao kuonyesha kwamba ni mali yao...

Kwa Mu-afrika hata angekataa mwisho wa siku wangechukua kwa nguvu...; Scramble and Partition of Africa, Mu-afrika alikuwa hana Say... (Just a Pawn to be Sacrificed)

Tofauti na sasa wachache wanaamua kugawa mali-asili ya vizazi vijavyo kwa faida ya muda mchache
 
Hii mikataba kama kesi za ardhi tu za kipindi hiki
 
Msovero Usagara Novemba 29, 1884.
Kwa kweli. huu mkataba haukuwaacha salama Wasagara hadi leo. Uchumi wao ni duni sana, ni kama wametengwa na dunia vile. Pamoja na udongo wenye rutuba na mito mingi Kilosa ya Wasagara bado imebaki nyuma na wao wameamua kuwa kama Waswahili halisi. Nashukuru Mungu Wasagara wamenipa ekari 40 ktk kijiji kilichokuwa na Ikulu ya Chief wao (Msovero a.k.a Msowero wanavyoitamka leo). Huku Usagara tuna hadi kijiji cha Ulaya.
 
Kwa ninayoyaona anayopitia Zelensky, na yaliyowapata, Mkwawa, Abushiri wa Pangani, Songambele, Songea na wengine walionyongwa na Wajerumaini inawezekana kabisa chifu Mangungo alikuwa Genious.

Trump ndio Karl Peters mpya na Hitler wa kizazi hiki.
 
Hio Mikataba ilikuwa for the benefit ya hao wakoloni yaani wakibishana huko kati ya Muingereza, Mjerumani na tuseme Mfaransa (Kampuni zao) waweze kusema mimi nilipata mkataba kabla yako..., Hawa machifu it was an offer they could not refuse (utake usitake wanachukua)

Mbaya ni hawa wa sasa wanajua kabisa detriments wa wanayoyafanya na wala hawashurutishwi bali wenyewe sababu ya matumbo yao na shortsightedness wanapeleka kugawa mali ya urithi...
 
Mpaka sasa bado sijaona ulaghai popote. Mleta mada unadhani Chifu Mangungu hakuelewa hicho alichosainishwa?
Mimi ningekuelewa ikiwa ungekuja na maelezo ya Chifu Mangungo yanayoeleza mkataba alioutaka yeye.
 
Kina Mangungo bado wapo katika bara letu la Afrika...
Miaka zaidi ya 60 ya uhuru wa Tz bado tunakabidhi rasilimali za nchi kwa waarabu kwa jina la mwekezaji. Wanaokabidhi nchi sasa hivi wanajua kusoma tofauti na mangungo.
 
mpaka sasa hao wakina Ukubhoko kwa Malaso(Mkono wa damu) a.k.a Carl peter bado wapo, kina Mangungo bado wapo na kina Ramazan bado wapo kumbe hawa ni waenzi na enzi...Asante kwa kutukumbusha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…