Huu ndio mtiririko wa matokeo ya kidato cha nne toka 2009-HAKI ELIMU

bushman

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
2,412
Reaction score
747
[h=5]Ndugu, hebu oneni mtiririko wa matokeo ya kidato cha nne; tangu 2009. Mdau mmoja wa elimu kaweka kwenye mtandao.Tuna cha kujivunia?

2012 Form 4 results

DIV 1: 1,641 (0.4%)
DIV 2: 6,453 (1.6%)
DIV 3: 15,426 (3.9%)
DIV 4: 103,327 (26.0%)
DIV 0: 240,903 (60.1%)

2011 Form 4 results

DIV 1: 3,671 (1.09%)
DIV 2: 8,112 (2.41%)
DIV 3: 21,794 (6.84%)
DIV 4: 146,639 (43.60%)
DIV 0: 156,085 (46.41%)

2010 Form 4 results

DIV 1: 5,363 (1.53%)
DIV 2: 9,944 (2.83%)
DIV 3: 25,107 (7.14%)
DIV 4: 136,777 (38.9%)
DIV 0: 174,407 (49.60%)

2009 Form 4 results

DIV 1: 4,419 (1.78%)
DIV 2: 10,493 (4.21%)
DIV 3: 27,310 (11.2%)
DIV 4: 130,651 (52.61%)
DIV 0: 65,708 (26.46%)
(HakiElimu)[/h]KUNA CHA KUJIVUNIA HAPO SERIKALI,KULIKUWA NA SABABU YA KUZUIA HOJA BINAFSI YA MH.JAMES MBATIA?????
 
Yoooote chini ya utawala wa kuchakachua matokeo ya uchaguzi mkuu! laaana kuu itawapata tu!!
 
Utaona Serikali itakuja kukataa na kusema huu ni uzushi.

Hapa hakuna cha kujivunia zaidi Viongozi na Serikali wawajibike.


Lakini huwa wagumu sana kujiuzuru wenyewe mpaka hii Nchi iwe na kiama.
 
Tutegemee majibu mepesi kama haya kutoka kwa viongozi wetu........

Ninahisi hapa kuna watu wanatumiwa na maadui wa mshikamano na maendeleo endelevu yaliyoletwa chini ya uongozi makini na imara wa serikali inayoongozwa na chama tawala. Nchi hii imepiga hatua kubwa katika idara mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu. Ikumbukwe kwamba, wakati nchi inapata uhuru idadi ya wananchi waliokuwa na elimu ilikuwa ni 3%, leo hii kutokana na juhudi mahususi za serikali tunazungumzia 71%! Kutoka shule chache sana nchini wakati tunapata uhuru, leo hii tunazungumzia kila kata kuwa na sekondari na idadi ya watoto wanaoanza shule ni 97%! Haya ni maendeleo ya kutukuka na yanayohitaji pongezi kwa kila anayeitakia mema nchi hii bila kutumiwa na wapinzani wa kisiasa. Ubora wetu wa elimu uko juu kulingana na nchi nyingi jirani kama vile Burundi, Congo, Mafia, na visiwa vya Somalia.

Nchi hii imefanikiwa kutokana na uongozi imara na siasa mwafaka ambapo muungano wetu wa Tanganyika na visiwa vya Zimbabwe unasifiwa dunia nzima na ni mfano wa kuigwa kwa wale wasio na husda na hatua zetu kubwa za maendeleo tulizozifikia. Ninapenda kuchukua fursa hii kuwasihi wananchi wawe watulivu tunapopita kipindi hiki kigumu cha kiuchumi duniani. Mshikamano wetu uendelee ili kuhakikisha maisha bora kwa kila mtanzania. Tunawahakikishia watanzania kwamba matokeo ya mitihani ya taifa yataboreka tu pindi pale hali ya kiuchumi duniani itakapotengemaa. Tumeshaahidiwa na marafiki zetu wanaotupa misaada kwamba walimu wataweza kulipwa vizuri zaidi na watoto wataweza kupata uji wa sukari angalau kwa kuanzia wakiwa shuleni. Ni mategemeo yangu kuwa kwa pamoja tutafikia malengo yetu na kuvuka kipindi hiki cha majaribu kinachokabili nchi nyingi.

Asanteni sana kwa kunisikiliza. Makofi na vigelele tafadhali!
 
Mtu ana bachelor ya IT mnampa Waziri wa Elimu mnategemea nini peaneni2 c mnataka watoto wetu wame mamessenger na secretary wa watoto wenu mlowapeleka Oxford na Cambridge tena wamerudi na Lower utaskia mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu cjui nani nani......Balali au cjui nani nani.......Nundu
 
Mtu ana bachelor ya IT mnampa Waziri wa Elimu mnategemea nini peaneni2 c mnataka watoto wetu wame mamessenger na secretary wa watoto wenu mlowapeleka Oxford na Cambridge tena wamerudi na Lower utaskia mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu cjui nani nani......Balali au cjui nani nani.......Nundu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…